Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.
Kwa mujibu wa takwimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.
Lakini kukiwa na vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.
Idadi kubwa ya maambuizi imekuja wakati ambao rais Donald Trump akitegemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu.
Rais Trump alieleza namna alivyosikitishwa na idadi ya maambukizi.
Naye makamu wa rais Mike Pence alisema kuwa vipimo vya corona virus vipo sasa katika majimbo yote 50 na zaidi ya watu 552,000 wamefanyiwa vipimo.
Bwana Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawafahamu idadi ya maambukizi yaliyopo China, "Hamfahamu takwimu ya maambukizi yaliyopo China."
Bwana Trump alikuwa amekosolewa kwa taratibu alizoweka mpaka ifikapo sikukuu ya Pasaka, April 12.
Mipango yake inaonekana kugonga mwamba baada ya siku ya Alhamisi , maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kuonekana kusambaa kwa kasi nchini mwake.
Siku ya Alhamisi alitangaza kuwa Wamarekani inabidi warejee kazini , nchi inabidi irejee katika hali yake ya kawaida mapema iwezekanavyo.
"Tunaweza kuchagua upande ambao hauna maambukizi sana na kuanza kuwajibika."
Aliongeza: "Watu wengi niliposema mrejee katika shughuli zenu, mlinielewa vibaya" naona waliachana na suala la kuwa mbali, kuosha mikono, kushikana mikono na kila kitu ambacho kilizuiwa.
Ufafanuzi zaidi alihaidi kutoa wiki ijayo.
Source: BBC Swahili
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.