Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

VIFO VYA KWANZA VYATHIBITISHWA AFRIKA YA KUSINIHUKU WATU WAKIZUIWA KUTOKA NJE

Afrika kusini imetangaza vifo viwili vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya corona wakati taifa hilo likianza kutelekeza marufu ya kutoka nje wakati taifa hilo likiwa na maambukizi zaidi ya 1,000.
Jeshi la ulinzi na usalama la Afrika kusini limeanza leo kuhimiza utekelezwaji wa marufuku ya kutoka nje ikiwa ni hatua ya kupambana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
Mapema kabla ya kuanza kutekelezwa kwa agizo hilo foleni ndefu ya watu ilionekana kwenye maduka makubwa wakifanya manunuzi muhimu ili kujiwekea akiba wakati huu wa marufuku ya kutoka nje.
Afrika kusuni imeripoti kuwa na wagonjwa 1000 ikiwa ni idadi kubwa zaidi barani Afrika.
Jioni siku ya Alhamisi rais Cyril Ramaphosa alitembelea kambi ya jeshi kabla askari hao kuruhusiwa kuingia barabarani
''Nina watuma kwenda kuwalinda watu wetu na virusi vya Corona,"Aliyasema hayo akiwa amevalia sare za jeshi.
''Ni wakati mbaya kwa demokrasia yetu, lakini pia kwa historia ya taifa letu kwamba tutaifunga nchi yetu kwa siku 21 ili kupambana na adui asiyeonekana, virusi vya corona"
Maduka ya vyakula hayatafungwa ingawa maduka ya vilevi yamepigwa marufuku wakati huu wa siku 21 Waziri wa Polisi Bheki Cel amewataka raia wa Afrika kusini kuwa timamu bila vileo wakati huu wa marufuku ya kutoka nje.
Siku ya alhamisi kuliripotiwa misururu mirefu ya magari kwenye barabara kuu ya kutoka Johannesburg, licha ya agizo la serikali la kuwataka watu wasiende safari ndefu.
Maelfu walifurika kwenye vituo vya mabasi wakikusudia kutoroka mjini na kwenda kukaa na familia vijijini jambo ambalo linazua hofu kwamba huenda baadhi wakaenda kuwaambukiza jamaa zao vijiji hasa wazee.
Source: BBC Swahili

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top