Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KAMPUNI YA FILAM YA 5 EFFECT SASA KUSAMBAZA MOVIE ZAKE.

Kampuni Kubwa ya Uandaaji na utengenezaji wa sinema nchini ya 5EFFECT sasa imejitenga na Kampuni ya usambazaji ya STEPS. 5 EFFECT ambayo sinema zake zote zilikuwa zikisambazwa na STEPS sasa imeamua kujitegemea kwa kila kitu baada ya miaka mingi ya kuitegemea kambuni hiyo ya Wahindi.
Akiongea na MoDesign Mkurugenzi wa 5effect Wlliam J. Mtitu, Amesema" sasa ni wakati wa ukombozi, hatuwezi kuwategemea watu kila siku lazima tujitahidi kufanya mabadiliko ili kuweza kuleta changamoto zaidi katika tasnia hii." alisema Mtitu.
Filamu nyingi zilizotengenezwa na 5EFFECT zilikuwa zikisambazwa na Kampuni hiyo ya STEPS, kwa malipo ambayo yalikuwa ni makubaliano kati ya kambuni hizo mbili. lakini baada ya kuona kuwa kuna vitu ambayo haviendi sawa 5effect imeamua kujitegemea kwa kila kitu.
"... najua itakua vigumu kuanza kusambaza wenyewe lakini tutajitahidi mpaka tutaweza tu, kitu kikubwa tunachokiomba ni sapoti ya watanzania, watanzania wakituelewa nini tunataka kukifanya basi ninaimani tutafanikiwa..." alisema Mtitu.
Mtitu amesema kuwa tayari yupo kwenye utengenezaji wa sinema ambazo ataanza kuzisambaza mwenyewe na tayari zipo katika hatua za mwisho kwa hiyo anaomba watanzania wakae mkao wakula. Filamu hizo ni pamoja na MR. MKENGA NA OMEGA CONFUSION.
Mtitu na Uwoya katika moja ya matukio ndani ya filam ya MR. MKENGA

Ma bodyguard wa Mtitu katika moja ya misafara ya Mkenga ndani ya filam ya MR. MKENGA

Bodyguard wa Mkenga akimzuia Irene Uwoya Asimsogelee Mkenga ndani ya filam ya MR.MKENGA

Nna imani kabisa watanzania watazipenda sinema hizi kwa vile zimekuja katika mfumo wa kisasa zaidi na nisinema ambazo nimezitengeneza katika viwango vya hali ya juu vya utengenezaji wa sinema, na vile nawaamini watendakazi wangu kwa vile wanauwezo mkubwa katika mendani hii,.. ssitapenda kusema mengi bali ntahitaji tu watanzania wajionee wenyewe viwango katika sinema hizi mbili..." hayo ni maneno ya mtitu.
Harusi ya Brian na Omega ndani ya filam ya OMEGA kwa nyuma ni Dude akiwakata jicho
IRENE UWOYA kama OMEGA ndani ya filam ya OMEGA
Filam ya OMEGA CONFUSION imewakutanisha baadhi ya wasanii nguli wa filam nchini kama vile IRENE UWOYA(OPRA), KULWA KIKUMBA(DUDE), WILLIAM MTITU, MARIAM ISMAEL, AGHATA MARLEY na wengine wengi.
ni sinema yenye mvuto na iliyoandaliwa kimataifa zaidi  na ikiwa imetafsiriwa kwa Kiingereza (subtitles).
Filam ya MR. MKENGA, imewakutanisha tena wasanii IRENE UWOYA(OPRA), WILLIAM MTITU, MARIAM ISMAIL, MIRIAM ROBERT, WASIWASI MWABULAMBO wa CLOUDS FM na wengine wengi. MR. MKENGA ni sinema inayokuja tofauti kabisa na sinema zilizozoeleka na iko kimataifa zaidi.
ni sinema ambayo Mtitu ameigiza kama mgombea urais na Uwoya ni mke wake. ni full mchakato wa kuelekea ikulu.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top