Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ZARI AMFUNGUKIA DIAMOND PLATNUMZ LIVE BILA CHENGA

ZALI & DIAMOND

ZARI The Boss Lady; ni baby mama wa supastaa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz anayeiwakilisha vyema Tanzania ambaye ametema nyongo kwa kumchamba jamaa huyo laivu bila chenga.

Ikumbukwe kwamba, Zari; raia wa Uganda anayeishi nchini Afrika Kusini amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi ambao ni Tiffah Dangote na Prince Nillan.

 

Katika sehemu ya pili ya shoo yao ya Young, Famous and African inayoendelea kwenye jukwaa la Netflix katika Mtandao wa YouTube, Zari anapiga stori na mwigizaji Khanyi Mbau wa Afrika Kusini ambapo anamueleza kwamba aliona ni bora alee watoto wake mwenyewe kuliko kuwa na kinyongo na Diamond ambaye alimsaliti mara nyingi mno.

 

Mwishoni mwa sehemu hiyo ya pili ya shoo hiyo ndipo hapo Zari akawa uso kwa uso na Diamond ambapo anamchamba laivu akifunguka yote mazito ambayo hajawahi kufunguka.

 

Zari anamwambia Diamond kuwa aliwahi kuwaza kuwa na familia yake; kwa maana awe na Zari kama mke hapa na watoto wake hapa?

Hapo Diamond hakuwa na majibu na kumfanya Zari kuendelea kumpa somo kwamba alimkatia tamaa na kumfanya jamaa huyo atulie tuli!

 

Zari anamwambia Diamond: “Unaona ulivyojishusha kama hapa, hukuwahi kujishusha wakati ule tukiwa pamoja, ulikuwa unapanda juu sana, ulijiona staa mkubwa, lakini nadhani leo umeelewa ni hasara kiasi gani umesababisha.”
Zari anaendelea; “Nilikuwa na uwezo wa kupigwa risasi kwa sababu yako kwa jinsi ambavyo nilikuwa ninakupenda.
“Mimi na watoto tulikuwa tunashambuliwa Baba Tee (Diamond), tulikuwa tumechoka, hukutulinda, hukufanya chochote.”

 

Wakati wote huo Zari akiwa anafoka kwa hisia kali na kulengwalengwa na machozi, Diamond alikuwa anatazama pembeni na kujigeuza asijue nini cha kujibu kwa namna alivyomuumiza kutokana na usaliti aliomfanyia kiasi cha kuzaa nje ya uhusiano wake ambapo alizaa na Hamisa Mobeto.

 

Itoshe kusema kuwa, kwenye shoo hii, hasa sehemu hii ya pili, Zari amemtolea uvivu Diamond na kutoa kile kilichoukamata moyo wake juu ya mzazi mwenzake huyo, jambo ambalo hakupata kulifanya.
Kwa kufanya hivyo, wengi wanaamini kuwa, Zari atakuwa ametoa kitu kikubwa na sasa roho yake itakuwa kwatu kabisa.

IDRIS ELBA KUIGIZA KAMA JAMES BOND KATIKA 007 MPYA


PRODUCERS  wa filamu za 007 James Bond, Barbara Broccoli na Michael G. Wilson wamethibitisha kuwa Jina la Idris Elba ni miongoni mwa majina yaliyotajwa wakati wanaongea kuhusu mwigizaji wa kuigiza kama James Bond baada ya Daniel Craig kumaliza filamu yake ya mwisho ‘No Time to Die’.

 

Hii ni filamu ya 25 ya James Bond. Majina mengine yaliyotajwa kwenye mazungumzo hayo ni Tom Hardy, Henry Cavill na Regé-Jean Page.

 

Oktoba 2021 Elba alisema hatachukua kazi hio ila kuna wakati alifikiria na alikuwa na shauku ya kuigiza kama 007 James Bond. Elba ameshaonyesha uwezo mkubwa wa kuigiza kupitia show kubwa za tv kama Luther, The Wire na filamu ya The Suicide Squad.

MO Designtz


 

NAY AWACHANA LIVE WASANI WAPENDA MAGARI NA LEBO


KUTOKA kwenye insta story ya Rapa Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameandika; “Yani kujifanyaga mnawapa magari ooh label kubwa alau mkishindwana mna wapokonya magari yenyewe tena wasanii kwa wasanii.

 

“Ndio mjifunze wasanii wapenda magari ya bure wakati mna vipaji na wakati mkikomaa mnaweza kununua ya kwenu kwa hela zenu coz muziki huu una hela huu ndio maana wao wanaweza hata kuwadanganya na hayo magari na kuwadhalilisha kwa kuwapokonya... hunijui limeboa soon napiga tour najinunulia ligari langu lingine likubwa,” ameandika Nay.

Unahisi, Nay amelenga wasanii gani au label gani ambao wanawapa magari wasanii wao na kuwanyang’anya?..



HARMONIZE AACHANA NA MPENZI WAKE MZUNGU

Huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu ambaye ni raia wa Australia Bryana likawa limevunjika kulingana na mfululizo wa post zake kupitia insta story yake.

Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa tu baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Kajala.

Mbali na hayo mwanamuziki huyo ametangaza kuachia wimbo wake mpya siku ya kesho unaitwa ‘Mwaka Wangu’

DAVIDO NA WIZKID WAMALIZA BIFU


 WASANII wakubwa Barani Afrika na duniani, Ayodeji Ibrahim Balogun almaarufu kama  ‘Wizkid na David Adedeji Adeleke almaarufu kama ‘Davido’ wamemaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda na sasa hivi wakikutana ni amani kama inavyoonekana kwenye picha.

Hii imetokea jana baada nguli hao wa muziki barani Afrika kukutana club nchini Nigeria na kukumbatiana kwa furaha, jambo ambalo limeleta furaha kwa mashabiki wao pia kuona wakipatana tena na kuwa kitu kimoja.








HUU NDIO WIMBO MAALUM MSIBA WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI... NI SIMANZI NA MAJONZI...

 

NIMELALA NA BABA MKWE WANGU ZAIDI YA MARA12 NA SIKO TAYARI KUACHA...


Dunia hii inakoelekea sasa sio kuzuri kwani mambo mengi ya ajabu yanakuwa yakitokea kila kukicha na mengine ni ambayo hayakutakiwa kufanyika katika jamii zetu za kiafrika kulingana na mila na tamaduni zetu.

mwanamke moja ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa vile hakutaka ijulikane kuwa janga hili limetokea katika familia yao, amesema amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na baba wa mumewe kwa muda mrefu yaani amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Baba Mkwe wake na tayari walisha kutana kimwili zaidi ya mara kumi na mbili 12 na anasema hayuko tayari kuacha.

anasema kwa sasa wanapangilia kusafiri nje ya nchi na mpenzi wake huyo kwa muda kwa vile tayari amajigundua kuwa ni mjamzito, ujauzito aliopewa na huyo Baba Mkwe wake.

Safari hiyo imepangwa mahusui kwaajili ya kwenda kuvinjari zaidi lakini pia kuchoropoa ujauzito huo "... kwani siko tayari kuiletea aibu familiayangu..." amesema mwanamke huyo.

anasema Baba mkwe wake pamoja na kuwa ni mtu mzima tayari lakini anamuonekano wa kuvutia alafu anajua sana kuvaa kitu amabacho kinamvutia sana.

HIZI HAPA PICHA ZA MREMBO ANAYEDAI KUWA NA MIAKA 19 TU...


 Tunapowatazama warembo wa kiafrica ni lazima tummwagie sifa zote mwenyezi Mungu kwa uumbaji wake Bora, twaweza kusema wakati Mwenyezi Mungu anaumba warembo wa ki Africa alitenga muda maalum kwaajili ya uchongaji huo.


Beverly Thlako ni mmoja kati ya warembo wengi wa kiafrika wanaojizoleea sifa kwenye mitandao ya kijamii hasa mtandao wa Instagram, hivi karibuni Thlako ametupia picha kibao na kuutangaza umri wake kuwa ni miaka kumi na tisa tu (19) kitu ambacho wengi bado wamekitilia mashaka kulingana na muonekano wake.


Thlako ni Mbunifu wa mitindo, Model na Blogger kutoka South Africa mwenye umri wa miaka kumi na tisa (19) kama mwenyewe anavyojitangazia lakini ukimtazama anaonekana kama mwanamke wa makamo kidogo amaye yuko zaidi ya umri huo alioutaja.


Limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa warembo wengi wakiafrika kuficha umri wao na kujitangazia kuwa na umri mdogo tofauti na mionekano yao hii haijajulika inatokana na nini lakini ni jambo ambalo linatokea maranyingi kwa warembo wengi wa kiafrika.


Toa pia maoni yako au mtazamo wako kuhusiana na madai ya Thlako na muonekano wake, lakini pia ni nini maoni yako kulingana na hili swala la warembo wengi kuficha umri wao?.











KUTANA NA BINTU MREMBO ALIYEJIZOLEA UMAARUFU KUTOKANA NA UMBO LAKE...

 Hajia Bintu ndilo kjina lake, ni mrembo kutoka nchi ya Ghana aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia mitandao ya kijamii hasa mtandao wa Tik Tok kwa kuonesha umbo lake zuri lenye mvuto wa kipekee.

Bintu amekuwa akipost picha mbalimbali zinazoenyesha umbo lake na kusababisha kujipatia followers wengi na wengi wakisifia na kuvutiwa na umbo lake lilivyokuwa nzuri.


Warembo wengi wenye maumbo ya kuvutia wamekuwa wakijaribu kutupia picha kwa minajiri ya kutaka kushindana naye lakini bado Bintu anaongoza kwa kufuatiliwa sana na bado anaonekana mwenye mvuto zaidi.


KUTANA NA MAPACHA WANAOTAFUTA MWANAUME MMOJA WA KUWAOA,.. WAMETOKA KWENYE NDOA YA KWANZA.


 Enzi hizi kipindi cha mababu zetu na katika tamaduni za muafrika neno Ndoa ilikuwa ni kitu kilichokuwa kikichukuliwa kwa uzito mkubwa sana tofauti na ilivyo kwa sasa. Babu zetu walikuwa wanaheshimu sana kitu kinachoitwa Ndoa, kulikuwa na mipaka iliyokuwa inazuia watu kuoana.

katika enzi hizo ilikuwa hairuhusiwi ndugu kuoa katika ukoo moja, ilikuwa pia hairuhusiwi mtu kuoa mtu ambaye wanatoka katika koo moja, ilikuwa ni vigumu kwa mtu kuoa dada wa tumbo moja au hata binamu ilikuwa sio rahisi.

Lakini katika kizazi hiki cha sasa, vitu na mambo ya ajabuajabu hutokea tu, tena vitu ambavyo kwa mababu zetu havikuwahi kutokea.


Mapacha hawa wanaofanana waliamua kufanya kitu ambacho hakikuwahi kutokea kwa enzi za mababu zetu ambapo waliamua kuolewa na mwanaume mmoja na kuishi naye kwa furaha kabisa bila shida.
Olwethu na Owami, ni mapacha wanaofanana wanaoishi nchini South Africa, walilelewa na Babu na Bibi yao na walipokuwa walikuta wakiwa katika sanaa ya uigizaji katika vipindi mbalimbali vya Television mbalimbali huko South Africa.


Walipoamua kuolewa na mwanamme mmoja wote walisema kuwa walijikuta katika mapenzi ya dhati na mwanamme huyo hivyo kwa pamoja wakaamua kuolewa naye. lakini ajabu ni kuwa waliishi kwa miaka michache tu baada ya kuamua kutalikiana na mwanaume huyo.


baada ya kumtaliki mume wao, mapacha hao walikiri kuwa wanajuta kuolewa na mwanaume huyo na kwa sasa wako katika msako wa kumtafuta mwanamume mwingine atakaye waoa wote wawili kwa pamoja kwani hawataki kuolewa na wanaume tofauti, wao lengo ni wapate mwanaume mmoja  tu na bado wanamatumaini kuwa watampata. 


© Copyright MO Design
Back To Top