Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MAM'DOGO LISA SEHEMU YA 18



 ILIPOISHIA TOLEO LA 17

 ... "... Sasa tutafanyaje Hasina maana huyo hatoki hapo mpaka taarifa ya habari iishe..." aliendelea kuhoji mzee Bisu. Hasina hakuwa na jibu zaidi ya kukaa kimya na kuendelea kutafakari...

SASA ENDELEA NA SEHEMU YA 18

... hakuna kati yao aliyekuwa akiongea neno wote walizama katika lindi la mawazo. walikuwa wakitafakari ni jinsi gani watafanya Dennis aweze kutoka pale sebuleni na mzee Bisu apate mwanya wa kuchoropoka mle chumbani kwa Hasina bila kuonwa na mtu yeyote, na ikibidi atoke nje kabisa ili kuwajengea watu imani kuwa kweli alikuwa mazoezini.
wakiwa katika kuendelea kutafakari mara walimsikia Dennis akiongea na mtu pale sebuleni, walitega masikio na kusikiliza kwa makini, Hofu iliongezeka baada ya kugundua kuwa aliyejuwa akiongea na Dennis pale sebuleni alikuwa ni mama yake yaani Bi. pauline, Mzee Bisu alitamani ardhi ipasuke apite chini kwa chini atokee nje ya geti, kwani alihisi kuwa uwezekano wa yeye kutoka mle chumbani kwa hasina ulizidi kuwa mdogo sana kwani kitendo cha mke wake kuamka kingesababisha azidi kukaa mle ndani kwa muda mrefu sana.
baada ya muda walisikia mtu akitembea kuelekea mlango wa kile chumba walichokuwemo Hasina alichungulia mlangoni na kugundua kuwa aliyekuwa akiusogelea mlango ule ni mke wa mzee Bisu. alikurupuka na kumsogelea mzee Bisu kisha akatamka kwa sauti ya taratibu"
"... tumekwisha, mama anakuja kugonga mlango wangu..."
mzee Bisu alikurupuka na kukimbilia uvunguni mwa kitanda cha Hasina lakini ikawa vigumu kuweza kuingia kulingana na ukubwa wa mwili wake alafu kitanda kilikuwa kifupi, wakati akihangaika kuingia, mlango uligongwa na sauti ya Bi. Pauline ikasikika.
"... Hasina,.. we Hasina..."
"... Beee..."
Hasina aliitikia huku macho yake yakiwa kwa mzee Bisu aliyekuwa akiendelea kulazimisha kuingia uvunguni bila mafanikio.
"... we bado umelala mpaka saa hizi wakati jua lilishakuchwa?.." aliendelea kuongea Bi. Pauline akiwa palepale mlangoni.
"... hapana mama nilishaamka muda mrefu mama na kuja..."
"... sasa unafanya nini chumbani humo, toka basi..." aliongea Bi. pauline huku akianza kuondoka
"... nakuja mama..."
ni kama walikuwa wanakimbia mbio ndefu kwani walishusha pumzi kwa nguvu tena kwa pamoja na huku sauti ya kuhema ya mzee bisu ikitokea chini ya uvungu, ni baada ya kusikia hatua za Bi. pauline zikitokomea sebuleni. mzee Bisu alikuwa amefanikiwa kuingiza kichwa tu uvunguni, akatoka na kisha kuanza kujifuta vumbi. mapigo ya moyo yalikuwa bado yakimuenda mbio na kijijasho kikiwa kinamtoka, akamuangalia Hasina kisha akamwambia.
"... inabidi utoke, maana ukibaki humu mama yako atakuja tena na mara hii ataingia moja kwa moja..."
"... sasa wewe utafanyaje?..." alihoji hasina
"... wewe nenda mimi ntabaki hata kama ntachelewa kutoka lakini ukishafika nje tafuta ujanja wowote ambao unaweza kuufanya ili na mimi nitoke humu ndani..."
Hasina alitikisa kichwa kukubaliana na alichokisema mzee Bisu kisha akafungua mlango na kutoka, hakumkuta Bi. pauline ila Dennis alikuwa bado kakaa pale pale, alipitiliza moja kwa moja na kuingia jikoni ambapo alianza kupanga kazi za kufanya, haikuchukuwa muda Bi. pauline naye aliingia jikoni.
"... we Hasina leo unatatizo gani..." alihoji Bi. pauline mara tu baada ya kuingia jikoni.
"... sina tatizo lolote mama..."
"... we si nilikusikia ukiongea na kaka yako Dennis hapo sebuleni?... sasa mbona ulirudi tena kulala wakati unajua kuwa umechelewa kuamka?.."
"... sijarudi kulala mama nilikuwa na jiandaa..."
"... haya fanya fanya basi haraka, baba'ako saa hivi atakuwa anarudi kutoka mazoezini na yele akifika tu lazima ataanza kuulizia chai si unamjua tena?..."
"... haya mama..." aliitikia Hasina huku moyoni akisema. "ungejua mumeo hajaenda mazoezini yuko chumbani kwangu..."
baada ya kumaliza kilichomleta mle chumbani Bi. pauline alitoka. Hasina naye hakuendelea na kazi bali alisogeamlangoni kuchungulia ni wapi anaelekea mama huyo. alimshuhudia akipitiliza kwenye korido ya kuelekea chumbani kwao, alipotupa macho pale sebuleni tena alimuona Dennis naye akiinuka na kuanza kutoka nje huku akijinyooshanyoosha, hakufanya kosa alitoka haraka baada ya Dennis kupotelea nje akakimbilia moja kwa moja mlangoni kwake na kunyonga kitasa akaingia bila hata hodi.
kidogo amuue mze wa watu kwani alishituka sana akijuwa tayari amkutwa na mkewe.
"... utaniua we mtoto, mbona haujabisha hodi..." aliongea mzee Bisu huku akitweta.
hasina hakujibu wala kupoteza muda wa kuongeaongea tena, akamkurupusha
"... toka, toka haraka wote wameondoka..." aliongea hasina huku akihema kulingana na zile mbio fupi alizopiga mle ndani.
mzee Bisu hakupenda kupoteza muda, alichomoka kama mshale na kwenda kusimama katikati ya sebule.
wakati anafunga breki tu akakutanisha macho na mwanaye Dennis ambaye naye alikuwa ndo anaingia kutokea nje. kwanza Dennis alipata mshituko na kisha akabaki akimkodolea macho baba yake bila kuongea neno na akiwa kasimama palepale mlangoni akiwa kama kapigwa na soti ya umeme. mzee Bisu naye alikuwa akimuangalia mwanaye kama kuna kitu alikuwa anasubiria kusikia kutoka kwake
NINI KIMEMDUWAZA DENNIS JE, KAGUNDUA KUWA BABA YAKE ALITOKEA CHUMBANI KWA HASINA AU ANASHANGAA NINI?

USIKOSE SEHEMU YA 19

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top