Pic: Mawazo Malembeka
hizi ni Piramidi za udongo zinazopatikana katika hifadhi hii ya mambo ya kale ya Isimila. zipo taarifa kuwa Piramidi hizi zilitokana na mmomonyoko wa udongo enzi hizo za mababu. yaani miaka mingi sana iliyopita.
Pic Mawazo Malembeka
Inasemekana kuwa Piramidi hizi zilisababishwa na Volcano iliyolipuka maahali hapa na kusababisha mmomonyoko huo wa udongo uliosababisha maajabu haya. taarifa hizi hupata msisitizo kutokana na kuwa juu ya Piramidi hizi kuna udongo mgumu uliochanganyikana na mawe ujulikanao kama Lavers.
Pic: Mawazo Malembeka
inasemekana udongo huo ulijijenga kutoka na Magma au uji wa moto unaorushwa na Volcano kupoa na kusababisha udongo na mawe kuchanganyika na kutengeneza kitu kigumu sana juu ya Piramidi hizi.
Piramidi hizi zinaoonekana kama kiudongo kilichosimama na ambacho kinaweza kufanya mtu akiogope kwa minajiri ya kwamba kinaweza kumdondokea.
Pic: Mawazo Malembeka
kwa mtazamo kweli ukiangalia kwa haraka utadhani kwamba ni rahisi Piramidi hizi kudondoka kwa upepo au kwamba mvua ikinyesha yanaweza kumomoyoka na kudondoka, La hasha, Piramidi hizi zilishapigwa na upepo na mvua za mawe labda kwa mamia au na maelfu ya miaka lakini bado ziko imara.
katika Hifadhi hii ya isimila pia zipo zana na kale za mawe nyingi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani, ambazo hizi zilitumiwa na watu wa kale kama vifaa vya kuwindia kukata na kata kusagia nafaka, hapa na manisha visu, mapanga, mikuki, mashoka na kadhaliaka.
kama huamini ni vema ukatembelea hifadhi hii ujihakikishie ukweli wa maajabu haya ya Mungu katika nchi yetu ya Tanzania.
endelea kufuatilia ili ujue maajabu mengi ya Mungu katika Nchi yetu.
Picha zote na Mawazo Malembeka
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
1 Maoni:
INA HITAJIKA KAMA KIASI GANI KUWEZA KUITEMBELEA HIFADHI HHIYO.
ReplyPost a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.