Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli.
Takwimu zimeripotiwa hivi karibuni na
Kick it Out, zinaonesha kuwa Mario Balotelli ndiye mchezaji
aliyebaguliwa sana katika ligi ya Uingereza, huku mchezaji huyo akipokea
zaidi ya ujumbe 8000, asilimia 50 kati ya…
Takwimu zimeripotiwa hivi karibuni na
Kick it Out, zinaonesha kuwa Mario Balotelli ndiye mchezaji
aliyebaguliwa sana katika ligi ya Uingereza, huku mchezaji huyo akipokea
zaidi ya ujumbe 8000, asilimia 50 kati ya hizo zikiwa ni za kibaguzi.
Kick it Out wameripoti takwimu hizo za kushtua, ambao walibaini
kwamba raia huyo wa Itali (Mario Balotelli) alilengwa sana katika
mitandao ya Twitter huku mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck akipokea
ujumbe 1700 asilimia hamsini kati ya hizo zikiwa za kibaguzi.
Mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck.
Mshambuliaji mwenza wa Balotelli katika kilabu ya Liverpool Daniel
Sturridge pia alionekana kulengwa katika mitandao ya kijamii baada ya
kupokea ujumbe wa 1600 asilimia 60 ikiwa ni ujumbe wenye mwelekeo wa
kijinsia.
Utafiti huo pia umebaini kwamba kilabu ya Chelsea ndio kilabu
iliobaguliwa zaidi kwa ujumbe 20,000 huku liverpool ikiwa ya pili na
ujumbe 19,000 Arsenal ikiwa ya tatu kwa ujumbe 12,000 huku Manchester
City na Manchester United zikipokea ujumbe 11,000.
Endelea kuperuz modesigntz Beste wangu wa ukweli, na mimi ntaendelea kukuwekea kila story inayotua kwangu...
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZAIDI
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.