RIPOTI kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa rais huyo kugombea kwa awamu ya tatu.
Jenerali huyo alitimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.