Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

SHERIA YA UCHAGUZI: POLISI WAZINGIRA BUNGE LA SENETI...

Maseneta nchini Kenya wamelalamikia kutishiwa na polisi waliozingira majengo ya bunge la seneti.
Aidha, polisi waliweka vizuizi mbalimbali katika barabara ya kuingia bunge.
Maseneta hao waliokongamano kwa ajili ya kikao maalum cha kujadili sheria ya uchaguzi, wameeleza kughadhabishwa na hatua ya polisi kuwadhalilisha bungeni.
Wamejitetea kuwa polisi waliojihami walimiminika katika sehemu mbalimbali ya bunge, jambo lisilokuwa la kawaida.
"Tunalaani vikali hatua ya polisi kuzingira bunge la Seneti na yeyote aliyehusika kuwapa mamlaka ya kuzingira bunge siku hii, anastahili kuchukuliwa hatua". Alisema kiongozi wa waliowengi katika Seneti, Kithure Kindiki.
Hata hivyo wabunge hao walitofautiana huku wengine wakiunga mkono kuwepo kwa polisi.
Seneta kutoka mrengo wa serikali, Kipchumba Murkomen, alisifu hatua ya kuwepo kwa polisi hao. "Tujilaumu wenyewe kwa mienendo yetu, tunaingia bunge tukibeba visu, pilipili na hata firimbi,". "Wabunge wenzetu wanamtusi rais. Ni aibu".
Kauli yake ilipokea upinzani kutoka Seneta Profesa Anyang' Nyong'o. "Tunamuomba Seneta Murkomen asitufananishe wabunge,".
Seneta Hassan Omar alipendekeza kikao hicho kivunjwe hadi polisi watoke bungeni.
Siku kadhaa zilizopita, bunge la taifa hilo lilishuhudia vurugu baada ya wabunge wa upinzani kujaribu kumzuia spika Justin Muturi kuingia bungeni wakipinga mjadala wa kubadilisha sheria za uchaguzi.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top