MBUNGE wa Singida Mashariki ambaye pia Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, amekamatwa na Jeshi la Polisi, leo Machi 6, asubuhi katika maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam.
Lissu aliyekuwa amekwenda mahakamani hapo kusikiliza kesi yake nyingine ya uchochezi, amekamatwa nje ya mahakama hiyo mara baada ya kumaliza kusikiliza kesi hiyo.
Ofisa Habari wa Chadema Tumaini Makene, amethibitishwa kukamatwa kwa Lissu.
“Ni kweli Tundu Lissu amekamatwa alipokuwa akitoka mahakamani kusikiliza kesi yake. Polisi hawajaeleza kwa nini wamemkamata na huenda wamempeleka kwa Kamanda Simon Sirro kuhojiwa, hatuna taarifa zaidi tutawajuza,” alisema Makene.
jitihada za kumtafuta Tundu Lissu kwa njia ya simu zilizaa matunda ambapo amekiri kukamatwa na jeshi hilo.
“Nimekamatwa na polisi, wamenileta hapa sentro lakini mpaka sasa hawajaniambia kosa langu ni lililosababisha wanikamate,” alisema Lissu.
Tunaedelea kufuatilia, tutawajuza kila linaloendelea kuhusiana na kukamatwa kwa Lissu.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.