Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MWAKYEMBE APIGA STOP TUZO ZA MUZIKI NA MASHINDANO YA MISS TZ...


WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison
Mwakyembe amepiga marufuku uandaaji na uendeshwaji wa mashindano ya urembo (Miss Tanzania) na tuzo za muziki hapa nchini kutokana na ubabaishaji wa waandaaji wa mashindano hayo.

Mwakyembe amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji wa hali ya juu ambapo kwenye utoaji wa tuzo kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu na mitafaruku.

Ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo ni lazima zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipelekwe ofisini kwa waziri huyo.

”Kwa sasa tutanakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo, lakini tunataka tuzo ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa kubahatisha tu!”, alisema Mwakyembe.

Kwa mara ya mwisho mashindano ya Miss Tanzania yalifanyika mwaka 2016 ambapo ilichukua takribani miezi 6 kwa Kamati ya shindano la Urembo la Miss Tanzania kumpatia mshindi zawadi yake.
Kwenye tuzo za muziki waziri Mwakyembe amesema tuzo hizo zinahitaji marekebisho kwani zilikuwa zikitegemea watu wachache kiasi kwamba wakinuna basi hakuna tuzo.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top