Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KAJALA URAIANI - WEMA AMUOKOA KAJALA NA KIFUNGO

Msanii wa maigizo na Filam nchini KAJALA MASANJA, leo ameachiwa huru baada ya kulipiwa faini ya milioni 13 na msanii mwenziye WEMA ISAC SEPETU..
WEMA NA KAJALA BAADA YA KUACHIWA HURU
Kajala Masanja na mumewe, walishitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu na kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka hayo.
Kajala Leo ameachiwa huru baada ya kusota rumande kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alinyimwa dhamana kulingana na uzito wa kesi hiyo.
Hukumu yake imetolewa leo ambapo alitakiwa kutumikia kufungo kwa kipindi cha miaka 8 au alipie faini ya sh milioni 13.
WEMA SEPETU MKOMBOZI WA KAJALA
Siku zote unapokaa na watu vizuri mungu anakuwa upande wako. na kweli mungu hakumtupa mbali mkombozi kajitokeza na kumlipia faini hiyo ya milioni 13 na sasa yuko Huru.
WEMA SEPETU amabye siku zote anaonekana muhuni kwa watu wengi leo ameonesha makali yake na kumlipia faini msani mwenzie.
hili kweli ni jambo la kuigwa alilolifanya wema na mungu amjalie.
KAJALA MASANJA
Kajala masanja aliwahi kuwa mpenzi wa mtayarishaji maarufu wa mziki wa kizazi kipya P FUNK MAJANI ambaye sasa ni mke wa Faraji Chambo alitamba kwenye filamu nyingi za kibongo ikiwemo filamu ya Marehemu Steven Kanumba ya DEVIL KINKDOM.


BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top