Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MAMA KANUMBA AMWAGA MACHOZI STEPS

MAREHEMU STEVEN KANUMBA (THE GREAT)

Mama mzazi wa aliyekuwa nguli wa filam Tanzania Steven Kanumba au kanumba the Great Flora Mtegoa, amemwaga machozi live mbele ya ofisi za Steps kwa kile kinachodaiwa kuwa alinyimwa pesa za mwanaye.
Habari kutoka ndani ya Bongo Movie na zilizonyakwa na Mdaku wa MO Design zinasema kuwa mama the Great alikwenda Steps kuomba shilingi milioni 2  kwa ajili ya kuandaa kumbukumbu ya kifo cha marehemu Kanumba lakini akanyimwa.
inasemekana kuwa alipokwenda kuomba pesa hizo alikuwa akizunguushwa mara aambiwe njoo kesho mara njoo wiki ijayo mwisho wa siku baada ya kuona amesumbuliwa sana alishindwa la kufanya akajikuta ametoka nje ya ofisi na kumwaga machozi.
MAMA KANUMBA - FLORA MTEGOA
Habari zina sema kuwa mama huyo alikuwa na uhakika wa kupewa pesa hizo ukizingatia kuwa kazi nyingi za mwanaye ziko pale na hata hivyo inasemekana kuwa Steps waliahidi kufanya sherehe ya kumbukumbu ya kifo cha marehemu The great...
R.I.P Steven Kanumba...

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top