Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MO- MTAYARISHAJI WA FILAM MWENYE VIPAJI VINGI

MO
Tunapozungumzia jina MOSE P au MO P au MO ni majina mageni kwenye masikio ya baadhi ya watu lakini pia sio geni kwa baadhi ya watu. kama jina MOSE P ni jina ambalo liliwahi kusikika katika nyanja za muziki wa kizazi kipya kwa kipindi fulani alafu likatoweka, kwa wale wanaokumbuka Wimbo kama Harusi ya kaka, Kadenti na Nyingine, watakuwa familia sana na jina hilo.
majina haya matatu ukijumlisha na jina halisi la MUSSA SIKABWE, ni majina ya PRODUCER anayebeba vipaji vingi sana katika kichwa chake japo watu wengi hawalifahamu hilo ukilinganisha na kuwa yeye mwenyewe hapendi kujionesha kwa watu kuwa anavipaji hivyo.
jamaa huyu kwanza ni mwana muziki aliye kamilika,  kwani anaweza kuimba vizuri na kupiga karibia vyombo vote vya muziki, kuanzia magitar, kinanda na vingine, alishawahi kuimbia baadhi ya bendi za kipindi hiko kama vile BICO STARS kwa wale wanaoikumbuka, NINA MUZIKA, BANA MAQUIS na nyingine ikiwemo kupiga mziki wa Hoteli yaani Squincer.
 Mali na kuimba muziki huyu jamaa ni mtayarishaji mzuri sana wamuziki nikiwa na maana ya PRODUCER. ni mtayarishaji amabaye alishapitia katika studio nyingi  kama METRO STUDIO, NASH RECORS, DREAMS ENTERTAINMENT, CMK PRODUCTION CHUWA RECORDS ya Morogoro na nyinginezo lakini tatizo la huyu jamaa huwa hapendi kujitangaza. huyu jamaa ndio mwalimu wa Producer ECK wa Eck Production.
ECK

Mbali na kuwa Mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki pia jama MO ni Producer mzuri sana wa filam.
Anaanda na kutayarisha sinema.
1. ni mwandishi mzuri wa Hadithi za sinema
2. ni mwandishi mzuri wa Script
3 ni mpigapicha mzuri wa sinema
4. ni Editor mzuri sana wa sinema
katika medani hiyohiyo ya sinema pia anafanya craphics na fx.
ameshafanya sinema nyingi pia yeye ndiye alikuwa editor wa vipindi vilivyokuwa vikirushwa na TBC vya BONGO DAR ES  SALAAM vya msanii KULWA KIKUMBA au DUDE na pia ameshirikishwa kuandaa sinema nyingi kama vile WRONG FAITH, TRUE FAITH, NGUMI YA MARIA, MAY MONEY IS MAY DEATH nanyingine nyingi, na sasa yupo katika Editing ya filam mpya ya mtitu inayowahusisha wasanii kama IRENE UWOYA, DUDE, MTITU na wengine wengi iitwayo OMEGA.
tukiachana na mambo ya filam jamaa ni muandishi wa habari na mtangazaji. Katika medani hiyo ya habari jamaa anfafanya vifuatavyo:
1. anauwezo wa kutafuta news
2. anauwezo wa kuedit news
3. anauwezo mzuri sana wa kutangaza ( radio na TV)
4. ana uwezo mkubwa wa kufanya Voice over ya matangazo mbalimbali
5. ni Sound producer mzuri wa Radio, anaproduce matangazo na Jingles.
alishawahi kufanya kazi na vituo vya habari kama vile kituo cha C2C, PASSION FM,  ITV RADIO ONE na CAPITAL RADIO AN' TV
Pia aliwahi kuchukuliwa na ABOUD radio an' Tv kwa ajili ya kuwatengenezea mambo madogo madogo kama vile Idents na graphics za tv jingles za radio na mengine.
jamaa pia ano uwezo mkubwa wa kutengeneza posters, covers za cd na mambo mengine yanayohusu graphics.
kweli jamaa huyu ni kichwa sana.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top