Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MFAHAMU VIZURI ACTOR WILL SMITH

je unamfahamu vizuri Will Smith? ni msanii mmarekani mweusi mwenye mbwembwe na vituko vingi katika kazi zake zote kuanzia muziki hadi sinema.

Will Smith ni:  actor, Rapper pia Producer


Will Smith alizaliwa Marekani jimbo la Philadelphia, Pennsylvania tarehe 25 mwezi september mwaka 1968 sasa ana umri wa miaka 44.
Will Smith anaishi na mkewe wa pili amabye ni Jada Pinkett Smith na ni baba wa watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike.
mwaka 1992 alioa mke wake wa kwanza ambaye alizaa naye mtoto aitwaye Willard Crhistopher maarufu kama Trey. mke huyo alikuwa akijulikana kwa jina la Sheree Zampino,
lakini ndoa yao ilidumu kwa kipindi cha miaka mitatu. mwaka 1995 waliachana na ndipo kwaka 1997 akamuoa Jada Pinkett ambaye mpaka sasa wana watoto wawili ambao ni Jaden Christopher syre (Jaden Smith - Born 1988 ) na Willow Camille Reign ( Willow Smith - Born 2000 )
Mpaka kufikia hapo alikofikia, Will Smith alianza kama MC wa kwenye matamasha ya Hip Hop na baadaye akachukuliwa na kituo cha NBC Television ambacho alifanya nacho mkataba katika kipindi cha The Fresh Prince of Bel-Air kipindi ambacho kilirushwa kwa miaka sita. na ndipo ambapo jina lake la Fresh Prince lilikozaliwa.
wakati huohuo alipewa Scene katika Drama iliyojulikana kama Six Degrees of Separation ambapo alifanya vizuri na ndipo akapewa na fasi ya kucheza Action Movie ya kwanza iliyojulikana kama
Bad Boy.
Baada ya hapo mtililiko wa kazi za sinema ukatiririka, ambapo mwaka 1996 alicheza katika sinema kama. Independence Day, mwaka 1997: Men in Black ambapo alicheza kama Agent J, mwaka 1998 alicheza Enemy of the State, mwaka 1999 akapewa role katika The matrix. Mwaka 2006 aliingizwa katika rekodi za Guinness Book of Wold. mwaka 2007 ikaachiwa filamu yake nyingine iliyoitwa
I am Legend ambayo alicheza na mwanaye Willow Smith . vilevile zipo sinema nyingine nyingi alizocheza kama Hangkock, Men in Black III na nyingine nyingi, inasemekana vile vile kuna sinema sajest kucheza na Rais wa Marekani ambayo haijapewa jina ila inafikiriwa kuitwa The Last Pharaoh but akaambiwa kuwa mpaka kipindi cha Uraisi wa Obama kipite. na sasa Smith na mwanaye wamekamilisha kupiga picha za After Earth ambayo itaachiwa mwaka huu wa 2013

Pamoja na kucheza sinema nyingi pia alifanya muziki na kushirikiana na wasanii kama T.I na the GAME. pia alifanikiwa kutoa album aliyokwenda kwa jina la Lost and Found.

Inasemekana kuwa katika kampeni za kugombea urais za Barack Obama, alichangia kiasi cha pesa ili kufanikisha kampeni hizo.

Will Smith na familia yake wana makazi Miami Beach, Florida, Los Angeles, Stockholm, Sweeden na Philadelphia.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top