Aliyekuwa Meneja wa Mwimbaji Nguli wa Muziki wa injili nchi Rose Muhando, Nathan Wami Mwaluganje, amekamatwa kwa kosa la Kitapeli yaani kusambaza Album mpya ya Rose Muhando iliyochini ya Kampuni ya Msama Promotion.
|
Nathan Wami Mwaluganje (Aliyekuwa Meneja wa Rose Muhando |
|
Nathan Wami alikamatwa baada ya utapeli wake kugundulika na mashuhuda au wasamalia wanaopenda maendeleo ya Wasanii kutoka Dodoma na kumtaarifu moja kwa moja Msama ambaye bila kuchelewa alimsweka ndani.
|
Mkurugenzi wa Msama Promotion |
Habari zaidi zinasema kuwa kwa mara ya kwanza Albamu hiyo ya Rose Muhando inayokwenda kwa jina la KAMATA PINDO ilianza kwenda kusambazwa Kenya ambapo kwa mara ya kwanza alipelekewa msambazaji wa huko ajulikanaye kwa jina la REHEMA, lakini akaitilia masahaka na kuachana nayo. matapeli hao hawakuishia hapo walimpelekea msambazaji mwingine wa Kenya aitwaye WISDOM, naye akaitilia mashaka ambapo alimpigia simu Msama.
|
Rose Muhando akiwa Jukwaani |
Habari zinaendelea kusema kuwa baada ya Msama kupigiwa simu alimuonya Nathan kwa vile ni Rafiki yake na mtu ambaye hufanya kazi pamoja, alimuonya na kumuambia asiendelee na mchezo huo. lakini baada yakushindwa kuiuza Albam hiyo Kenya, Nathan na kundi lake waliamua kuisambaza Albamu hiyo kiubishi wakianzia Dodoma, lakini kwa bahati mbaya siri ikavuja.
akizungumza na waandishi wa habari Rose Muhando alithibitisha Wizi wa kazi yake, na akasema kuwa Nathan kweli amekamatwa na yuko rumande, akasema pia kuwa hakuna ubishi kwa vidhibiti vyote vipo na bado wanaliachia jeshi la polisi lifanye kazi yake.
Albamu ya KAMATA PINDO inatarajiwa kuzinduliwa Tarehe 03/08/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.