ILIPOISHIA SEHEMU YA 21
...aliliendesha gari mpaka akatokea mtaani kwake. akiwa ndio anakata kona ya kuingia katika mtaa huo akamuona Mke wake Bi. Pauline na yeye ndio anatoka getini kwake, akafunga breki za ghafla na kulipaki gari pembeni kwa haraka...
SASA SHUKA NA SEHEMU YA 22
... Lakini alikuwa kachelewa kwani Bi. pauline alishaliona gari na kutambua kuwa ni gari la mumewe,. akaanza kuelekea kule lilikopaki gari lile alilolitambua kabisa kuwa ni la mumewe. akiwa ndani ya gari Mzee Bisu alianza kutafakari ni nini amdangaye mkewe, kwani haijawahi kutokea hata siku moja akarudi nyumbani mapema kiasi kile hasa mwanzoni mwa wiki kama hivyo, kichwa chake kikawa kinafanya kazi ya haraka ili kupata jawabu la kumdanganya mkewe ambaye hakutarajia kama atamkuta mida hiyo na ambaye ndio alikuwa analikaribia gari tena akimkodolea macho. ghafla wazo moja likampita kichwani mwake, hakupenda kufikiria mara mbili, akanyanyua simu yake na kuiweka sikioni akaanza kuongea kwa sauti tena kwa kufoka.
"... na sipendi tena ujinga huu ujitokeze siku nyingine, unanisikia... mara kwa mara nakuambieni kuwa makini katika kazi lakini hampendi kunielewa... hatimaye mnaanza kupoteza mafaili ofisini huu si uzembe..."
wakati akiendelea kuongea kwa jazba hivyo mkewe Bi. Pauline alikuwa keshafika pale alikopaki gari, akasimama dirishani bila kumuongelesha akimuacha amalize maongezi yake, Mzee Bisu naye hakutaka kuipoteza nafasi hiyo ya mchezo huo aliomchezea mkewe bila kujijua, akaendelea kuongea kwa hasira.
"... nawambia tena kwa mara nyingine,.. uzembe kama huu ukijitokeza tena, wote vibaruwa vitaota nyasi... sipendi kuendelea kufanya kazi na watu wasionielewa na wasiokuwa makini katika kazi zao..." akakata simu na kumuangalia mkewe huku bado sura yake ikiwa imejenga makunyanzi ya hasira, Bi Pauline naye akawa anamtazama kwa macho ya kuuliza kulikoni, na kweli hakuchelewa akampachika swali hilo.
"... vipi tena baba dennis?.."
".. aghh... si hawa wajinga wanafanya kazi bila kuwa makini hatimaye wanapoteza mafaili ofisini..." aliongea Mzee Bisu huku akiwa bado amejenga makunyanzi ya hasira usoni kwake. lakini mkewe alikuwa bado na maswali ya kumuuliza, hata yeye alilijua hilo hivyo akajiweka tayari kukabiliana nayo, lakini akiwa na uhakika kuwa kwa uongo ule alioutengeneza tayari atakuwa alishamlainisha mkewe.
"... una maanisha wafanyakazi wako?.."
"... ndiyo... unafikiri nani mwengine?.." alijibu na kisha kumalizia na swali ambalo halikupata jibu badala yake akapachikwa swali jingine.
"... sasa wafanyakazi wamepoteza mafaili ofisini alafu wewe uko huku nyumbani saa hizi kulikoni?.." lilikuwa ni swali ambalo alikuwa akilitarajia kwa muda mrefu na ndio maana ya kutengeneza uongo wote ule wa simu hivyo akalijibu swali hilo kama ifuatavyo.
"... hilo lililopotea ni faili la mteja ambaye mpaka saa hizi tunavyozungumza hapa yuko pale ofisini kwa ajili ya kazi yake, bahati nzuri ni kwamba faili hilo nilikuwa na nakala yake hapa nyumbani ndio maana nimerudi haraka, sasa nakata tu kona hii eti wananipigia simu kuniomba msamaha kwa uzembe wao... ndio nikapaki niongee nao... na ... wewe unakwenda wapi?.." aliongea ka kirefu kisha akamalizia kwa swali ili kukazia uongo wake asionekane kuwa alikuwa na wasiwasi. lakini uongo wake ulizama vizuri sana kichwani kwa mkewe na ambaye alikosa cha kuongeza badala yake akaanza kuoto maoni. "... dah ila hapo baba Dennis ulicheza,.. sasa kama usingekuwa na nakala si biashara ilikuwa imeharibika..." moyoni Mzee Bisu alishangilia kwa uongo wake kukubalika bila kikwazo. akamuangalia tena mkwe na kurudia swali lake.
"... unakwenda wapi?.." lilikuwa ni swali lenye maana kubwa sana kwake baada ya uongo wake kukubalika, ni swali ambalo lingemuhakikishia usalama wake kwa kile alichokuwa anakwenda kukifanya.
"... nakwenda mnazi mmoja kwa mama Siwa kuhusiana na yale mambo yangu niliyokuambia..."
"... ah yale mambo yenu ya vitenge?.."
"... ndiyo..."
"... sawa ngoja mimi niwahi nyumbani nichukue hilo faili nimuwahi mteja ofisini..." aliongea Mzee Bisu akilitia gari moto. lakini mkwe akuonesha kuondoka na alionekana bado kuna kitu alitaka kuongea, hilo Mzee Bisu aliliona na akabaki kumkodolea macho.
"... nini?.." aliuliza huku akiwa kamkodolea macho mkewe
"... sasa kama ni kuchukua faili tu sinikusubiri tu ili unipitishe pale mnazi mmoja alafu ndo uunganishe ofisini?.." ni swali ambalo Mzee Bisu hakulitarajia kabisa hivyo likamtia kigugumizi kulijibu. lakini kabla hajajua ajibu nini, mkewe akaendelea kumuweka katika wakati mgumu zaidi.
"... hata usiponipeleka mnazi mmoja kabisa, ukiniacha pale Hakiba itakuwa vizuri..." Mzee Bisu alijikuta akinyong'onye ghafla, kwani alikuwa ameplani amdanganye kuwa yeye hataki kupita kokote kwani anaharaka sana kitu ambacho mkewe alikuwa naye kakigundua akaamua kumwambia hivyo. kwani ofisi ya mzee Bisu iko posta mpya hivyo asingeweza kupita mnazi mmoja. Mzee Bisu akajikuta katika wakati mgumu sana na kichwa chake kikaanza kufikiria kwa haraka amjibu nini mkewe huyo aliyeonekana kutaka kumuharibia mpango wake wa siku hiyo na ambao hakutaka kabisa kupoteza nafasi hiyo. kila alipokuwa akifikiria anachokwenda kukufanya mwili ulimsisimka na kujikuta akichukia kukutana na mkwe pale, akatamani amjibu hovyo lakini akagundua kuwa akifanya hivyo mkewe atamtilia wasiwasi, akaamua kutengeneza uongo mwingine unaofanana na ukweli. kwa sauti iliyotulia na isio na wasiwasi akamjibu mkewe.
"... year, lilikuwa ni wazo zuri lakini, hili faili limeambana na taarifa fulani hivi ya kipolisi kwa sababu hii ni biashara ya pesa nyingi, hivyo inanibidi nipite Ostarbay Polisi kwa ajili ya kuchukua nakala nyingine ya taarifa hiyo ya kipolisi kwa ajili ya kuambatanisha tena na faili hilo. aliongea Mzee huyo aliyekusudia siku hiyo lazima afanye kile alichokikusudia kwa kutengeneza uongo. aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa shati na kutoa noti kadhaa za elfu kumi kumi na kumpa mkewe.
"... labda tufanye hivi, wewe kachukuwe taxi hiyo hapo ikupeleke, hii iwe kama adhabu yangu ya kushindwa kukupeleka mke wangu. Aliogea Mzee Bisu baada ya kuona texi moja iliokuwa inatokea mbele yake. bila kuongea neno Bi. Pauline alizipokea na kisha akaioneshea ile taxi ishara kwamba isimame naye akaanza kuifuata, lakini Mzee Bisu akamuita tena.
"... Mama Dennis,.." Bi. Pauline akamuangalia
"... umechukia?.."
"... hapana, ni chukie kwa nini wakati najua kabisa unahangaikia kazi ambayo ndio inatuweka mjini hapa!?." alijibu Bi. Pauline bila kuonesha kinyongo.
"... basi sawa..." waliaga na mkewe kisha Bi. Pauline akajipakia ndani ya taxi na kuondoka. Mzee Bisu alihakikisha taxi aliyopanda mkewe imepotea ndio naye akaliondoa gari na kuingia nyumbani kwake. alilipaki gari kisha akatoka tena getini kuchungulia na kuhakikisha kama kweli mke wake ameondoka. baada ya kujihakikishia usalama wake alirudi kwa mwendo wa haraka huku akiwa katengeneza bonge la tabasamu, alikuwa na furaha kubwa kwani alikuwa na uhakika kuwa mpango wake umekaa vizuri,. mwili ulikuwa ukimsisimka kila amfikiriapo Hasina. aliingia ndani kwake na kwenda kusimama katikati ya sebule iliyokuwa tupu. aliangalia huku na huku bila kuona mtu mle ndani, akageuka na kuuangalia mlango wa kuingilia chumbani kwa Hasina, akatabasamu kisha akaanza kutembea kuuelekea mlango huo, taratibu akakishika kitasa na kukinyonga mlango ukafunguka, huku akiwa kajenga tabasamu usoni kwake akaingiza kichwa kwa mtindo wa kuchungulia huku akiita.
"... mremboooo..."
lakini baada ya kicha chake kuzama ndani na kuangalia huku na huku aligundua kuwa chumba kilikuwa kitupu, Hasina hakuwemo...
Maoni na ushauri wako ni muhimu sana kwetu.... Sema chochote kuhusiana na Kisa Hiki.
NINI KITAENDELEA? USIKOSE SEHEMU YA 23
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.