Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MAAJABU YA TANZANIA 2 "KIMONDO" KUTOKA ANGA YA SAYARI YA MARS NA JUPITER

Tukiacha Vivutio vya Mapiramidi na Zana za Kale za Mawe zilizoko Iringa, Kivutio kingine na kinachowavutia watu ni KIMONDO kilichopo katika Mkoa wa Mbeya.

Pic: na Mawazo Malembeka
Inasemekana Kimondo hiki kilianguka kutokea katika anga la la sayari ya Mars na Jupita na kilidondoka miaka mingi sana iliyopita, lakini
kikagundulika mwaka wa 1930 mkoani Mbeya.
Inasemekana kuwa miaka ya kabla ya mwaka huo wa 1930 Jamii ya watu waliokuwa wakiishi kipindi hicho walipokigundua walikuwa wakikitumia kama Muungu, yani walikuwa wakikiabudu kama Mungu na kukitumia kwa matambiko mbalimbali kwa kuamini kuwa ni Mwamba wa ajabu.

Pic: na Mawazo Malembeka
inasemekana kuwa baada ya hapo Serikali ya Uingereza ilileta wa taalamu wa Miamba na ndipo ikagundulika kuwa ni Kimondo na sio Mungu, hiyo ikiwa ni katika mwaka huo wa 1930.
Katika utafiti huo uliofanywa na wataalamu walioletwa na Serikali ya Uingereza, iligundulika kuwa Kimondo hicho kilikuwa na mchanganyiko wa Madini matano ambayo ni"
1. Madini ya Chuma
2.Madini ya Nikel
3. Madini ya Copa
4. Madini ya Sulphat
5. Madini ya Phosphat
ugunduzi mwingine ni kuwa kiligundulika kuwa na uwezo wa kuvuta Tone 12.
Kimondo Hicho kwa mara ya kwanza kilikuwa kikihifandiwa chini ya utawala wa Chifu Mwamengo na kikaja tena kuhifadhiwa na Wakoloni wa Uingereza na kwa mara ya tatu sasa kinahifadhiwa chini ya Serikali ya Tanzania baada ya kupata Uhuru.

Usichoke kufuatilia makala hizi ili uweze kujua Mengi kuhusu Maajabu yanayopatikana Tanzania...
Picha zote na Mawazo Malembeka.


BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top