Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MTANZANIA ALIYEWAUWA KIKATILI WANAWE WAWILI HUKO AUSTRALIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA


Charles Mihayo mikononi mwa Polisi
Charles Mihayo (36) mzaliwa wa Tanzania ambaye mwezi April, 20,2014 aliwauwa watoto wake wawili wa kike nyumbani kwake  huko Melboune, Australia, amehukumi wa kifungo cha maisha.
Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na mkewe Mihayo kwa
hasira aliamua kufanya ukatili huo wa kukatisha maisha ya watoto wake mwenyewe, Savannah (4) na Indiannah (3) ili tu kumuumiza mkewe kama njia ya kumlipizia kisasi. inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.

Watoto Savannah na Indiannah ( marehemu)
Taarifa zinasema kuwa siku mauaji hayo yanafanika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo.baada ya kuwafikisha baba yao aliwafanyia shopping ya nguo mpya na viatu.
kabla ya kutenda ukatili huo wa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza mziki huku yeye mwenyewe akicheza nao kwa furaha. na katika video ambayo baadaye polisi waliiona, alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizawanunulia, na walifanya hivyo kisha Mihayo alikaa mbele ya kamera hio na kusema "...tutamuonesha mama kitu kingine dakika kumi zijazo" na kisha aliendelea kucheza nao hai alipowakandamiza kwa mto ( pillow) hadi kufa.
Baada a kufanya mauaji hayo aliwapigia simu mwenyewe ambao baada ya polisi kufika nyumbani kwake wakiwa mlangoni aliwaambia "... Tayari nimewaua... nimewauwa watoto wangu inabidi mumuulize huyu
(mama yao) sababu.
Polisi waliwakuta watoto hao wakiwa tayari wamefariki huku wakiwa wamevalishwa nguo na viatu vipya ambavyo walinunuliwa na baba yao siku hiyo. licha ya kuhukumiwa kifungo cha maisha Charles Mihayo anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top