Ni tukio la kusikitiha sana na kuhuzunisha, inasikitisha sana kuona jinsi binaadamu tume kuwa kama wanyama na kuuana kwa ukatili wa kiasi hiki.
Katika kijiji cha Songambele Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, watu wasiojulikana wamemvamia mwenyekiti wa Kijiji cha Songmbele na kumchinja kama kuku na kutenganisha kabisa kiwiliwili na kichwa ikiwa ni pamoja na kuzikata sehemu zake za siri ikiwemo na kumkata mkono wa kulia na kuukata mara mbili.
baada ya kukata viungo hivyo walivyovitaka, walivichukuwa na kuviweka ndani ya sifuria na kuanza kuvichemsha kama wachemshavyo supu au mhemsho.
Baada ya kufanya unyama huo wauaji hao walitokomea kusiko julikana.Polisi Wilayani Mlele wanaendelea na uchunguzi kubaini wakina nani waliohusika na tukio hilo na nini sababu ya unyama huu. tukio hili limetokea leo majira ya saa saba usiku
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.