Ni taarifa kutoka Dodoma ambapo tarehe 04.02.2015 askari Polisi Joseph Isack Swai ameuwawa huku chanzo chenyewe kikielezewa kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa chang’ombe juu Dodoma Mjini akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa OLIVER D/O BALTAZARI, MIAKA 52, CHAGA, MKAZI WA CHANG’OMBE JUU kuwa kijana wake aitwaye TISI S/O SIRILI MALYA ana mtesa mtOto wake mdogo wa miezi nane aitwaye VALERIAN S/O TISI MALYA na anahisi labda ameshamuua kwani motto huyo halii tena.
Polisi wamesema ‘alichofanya mtendaji ni kumpigia simu askari akaenda wakaongozana pia na kijana mmoja hadi anakoishi huyo TISI S/O SIRILI MALYA, walipofika askari aligonga mlango akijitambulisha kuwa yeye ni askari hivyo atoke nje.
Alichofanya mtuhumiwa huyo ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi nane kwa mkono mmoja miguu juu kichwa chini na kutaka kumkata kwa panga na kusema ‘namkata shingo na sitaki kuona mtu‘
Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo na alipomrukia mtuhumiwa kwa bahati mbaya aliteleza na kumkata kichwani askari na akadondoka chini kutokana na jeraha kubwa ambapo hata hivyo mtuhumiwa aliendelea kumkatakata ambapo Mtendaji na kijana waliyekuwa naye ambaye ni mratibu wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliwabidi kukimbia huku na kupiga kelele kuomba msaada.
Mtuhumiwa baada ya kufanya hicho kitendo alikimbia huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu akiwa na panga mkononi.
Askari huyu muda mfupi kabla ya tukio hili alikuwa ametokea katika kituo cha Redio cha Dodoma FM kwa ajili ya kuandaa kipindi cha kuielimisha jamii juu ya ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) tunapoelekea kipindi cha uchaguzi, kwani mbali na kazi anazofanya mojawapo ni kushiriki katika vipindi vya kutoa elimu ya Polisi Jamii hapa mkoani Dodoma.
Msako bado unaendelea ili kuweza kumtia nguvuni mtuhumiwa huyu aliyesababisha kifo cha askari wetu wakati alipojitolea maisha ya ili kumwokoa huyo mtoto mdogo.
Polisi wanasema ‘tunazidi kuomba msaada wa wananchi popote pale watakapomuona TISI S/O SIRILI MALYA, MIAKA 29, MCHAGA ambaye ni maji ya kunde, mwembamba, siyo mrefu sana saizi ya kati alikuwa amevaa suruali rangi ya blue iliyopauka na T-Shirt rangi ya dark blue na kofia nyeupe yenye alama nyekundu ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani.
Imetolea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi – Misime D.A (SACP)
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.