Akizungumza na nasi wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata yeye ni makombo na bado anakula makombo?
“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond na kuongeza:
“Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya msingi ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na hiyo.”
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.