Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

NIMELALA NA BABA MKWE WANGU ZAIDI YA MARA12 NA SIKO TAYARI KUACHA...


Dunia hii inakoelekea sasa sio kuzuri kwani mambo mengi ya ajabu yanakuwa yakitokea kila kukicha na mengine ni ambayo hayakutakiwa kufanyika katika jamii zetu za kiafrika kulingana na mila na tamaduni zetu.

mwanamke moja ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa vile hakutaka ijulikane kuwa janga hili limetokea katika familia yao, amesema amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na baba wa mumewe kwa muda mrefu yaani amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Baba Mkwe wake na tayari walisha kutana kimwili zaidi ya mara kumi na mbili 12 na anasema hayuko tayari kuacha.

anasema kwa sasa wanapangilia kusafiri nje ya nchi na mpenzi wake huyo kwa muda kwa vile tayari amajigundua kuwa ni mjamzito, ujauzito aliopewa na huyo Baba Mkwe wake.

Safari hiyo imepangwa mahusui kwaajili ya kwenda kuvinjari zaidi lakini pia kuchoropoa ujauzito huo "... kwani siko tayari kuiletea aibu familiayangu..." amesema mwanamke huyo.

anasema Baba mkwe wake pamoja na kuwa ni mtu mzima tayari lakini anamuonekano wa kuvutia alafu anajua sana kuvaa kitu amabacho kinamvutia sana.

HIZI HAPA PICHA ZA MREMBO ANAYEDAI KUWA NA MIAKA 19 TU...


 Tunapowatazama warembo wa kiafrica ni lazima tummwagie sifa zote mwenyezi Mungu kwa uumbaji wake Bora, twaweza kusema wakati Mwenyezi Mungu anaumba warembo wa ki Africa alitenga muda maalum kwaajili ya uchongaji huo.


Beverly Thlako ni mmoja kati ya warembo wengi wa kiafrika wanaojizoleea sifa kwenye mitandao ya kijamii hasa mtandao wa Instagram, hivi karibuni Thlako ametupia picha kibao na kuutangaza umri wake kuwa ni miaka kumi na tisa tu (19) kitu ambacho wengi bado wamekitilia mashaka kulingana na muonekano wake.


Thlako ni Mbunifu wa mitindo, Model na Blogger kutoka South Africa mwenye umri wa miaka kumi na tisa (19) kama mwenyewe anavyojitangazia lakini ukimtazama anaonekana kama mwanamke wa makamo kidogo amaye yuko zaidi ya umri huo alioutaja.


Limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa warembo wengi wakiafrika kuficha umri wao na kujitangazia kuwa na umri mdogo tofauti na mionekano yao hii haijajulika inatokana na nini lakini ni jambo ambalo linatokea maranyingi kwa warembo wengi wa kiafrika.


Toa pia maoni yako au mtazamo wako kuhusiana na madai ya Thlako na muonekano wake, lakini pia ni nini maoni yako kulingana na hili swala la warembo wengi kuficha umri wao?.











KUTANA NA MAPACHA WANAOTAFUTA MWANAUME MMOJA WA KUWAOA,.. WAMETOKA KWENYE NDOA YA KWANZA.


 Enzi hizi kipindi cha mababu zetu na katika tamaduni za muafrika neno Ndoa ilikuwa ni kitu kilichokuwa kikichukuliwa kwa uzito mkubwa sana tofauti na ilivyo kwa sasa. Babu zetu walikuwa wanaheshimu sana kitu kinachoitwa Ndoa, kulikuwa na mipaka iliyokuwa inazuia watu kuoana.

katika enzi hizo ilikuwa hairuhusiwi ndugu kuoa katika ukoo moja, ilikuwa pia hairuhusiwi mtu kuoa mtu ambaye wanatoka katika koo moja, ilikuwa ni vigumu kwa mtu kuoa dada wa tumbo moja au hata binamu ilikuwa sio rahisi.

Lakini katika kizazi hiki cha sasa, vitu na mambo ya ajabuajabu hutokea tu, tena vitu ambavyo kwa mababu zetu havikuwahi kutokea.


Mapacha hawa wanaofanana waliamua kufanya kitu ambacho hakikuwahi kutokea kwa enzi za mababu zetu ambapo waliamua kuolewa na mwanaume mmoja na kuishi naye kwa furaha kabisa bila shida.
Olwethu na Owami, ni mapacha wanaofanana wanaoishi nchini South Africa, walilelewa na Babu na Bibi yao na walipokuwa walikuta wakiwa katika sanaa ya uigizaji katika vipindi mbalimbali vya Television mbalimbali huko South Africa.


Walipoamua kuolewa na mwanamme mmoja wote walisema kuwa walijikuta katika mapenzi ya dhati na mwanamme huyo hivyo kwa pamoja wakaamua kuolewa naye. lakini ajabu ni kuwa waliishi kwa miaka michache tu baada ya kuamua kutalikiana na mwanaume huyo.


baada ya kumtaliki mume wao, mapacha hao walikiri kuwa wanajuta kuolewa na mwanaume huyo na kwa sasa wako katika msako wa kumtafuta mwanamume mwingine atakaye waoa wote wawili kwa pamoja kwani hawataki kuolewa na wanaume tofauti, wao lengo ni wapate mwanaume mmoja  tu na bado wanamatumaini kuwa watampata. 


HAWA HAPA MASTAR WA KENYA WALIOAMUA KUJITANGAZA HADHARANI KUWA NI MASHO*A

 Ongezeko la watu mbalimbali kujitokeza na kujitangaza hadharani kuwa wana mahusiano ya jinsia moja, yaani Gay, Lesbian, Bisexual, linazidi kuwa kubwa siku baada ya siku hasa kutokana na hamasa zinazo sadikika kutokana na mitandao ya kijamii ambapo watu wa jamii hizo huzidi kuhamasishana.

Kwa sasa kuna iddi kubwa ya baadhi y mastar kutoka nchini Kenya walioondoa kabisa uoga na wasiwasi wao na kujivisha ujasiri kisha kuamua kujitangaza hadharani kuwa nawao wako katika mahusiano hayo.

YUPO MAKENA NJERI


Huyu Makena Njeri alikuwa muigizaji mzuri sana wa Runinga aliyeigiza kwa viwango vya hali ya juu katika Tamthilia ilitohuwa inajulikana kipindi hicho kama TAHIDI. Makena amekuwa akizungumziwa sana katika mitandao kulingana na muonekano wake wa mavazi ambapo amekuwa akipendelea kuvaa ma vazi ya kiume zaidi ya ya Kike lakini pia kuligana na Skendo ya kusalitiwa na mpenzi wake wa kike.


CHIMANO


Chimano ni mmoja wa wanamuziki wanaounda kundi linalofanya vizuri sana nchini Kenya la Sauti Sol, Yeye pia alijitokeza Hadharani na kutangaza ukweli kuhusiana na yeye kuwa Sho*a ambapo alipokea matusi mengi na maneno mabaya kutoka kwa watu mbalimbali walioiona post yake hiyo katika mtandao wa Twitter, lakini pia haikumjengea mtazamo mzuri kwa mashabiki wanaomsapoti katika taaluma yake ya Muziki lakini yeye hakujali.
"... mimi ni Sho*a, mtanikubali au mtani kataa?.. nilihitaji kupata mudda mzuri.."

AUDREY MBUGUA

Huyu ni mmoja kati ya waliojitangaza mapema kabisa kama ma Sho*a nchini Kenya. Alikuwa akitambulika kwa jina lake halisi ambalo ni hilo Andrew Mbugua kabla ya kuamua kujibadilisha jinsia kitu kilichopelekea abadili na Jina lake na kuitwa Audrey Mbugua

Andrew Mbugua katika muonekano wake wa Kike kama Audrey Mbugua








TWIGA WAMO HATARINI KUANGAMIA...

Twiga wamepungua sana duniani katika kipindi cha miaka 30 iliyopita na kwa sasa wanakabiliwa na hatari ya kuangamia.
Idadi ya twiga duniani imeshuka kutoka 155,000 mwaka 1985 hadi 97,000 mwaka 2015 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi wa mambo asilia (IUCN).
Idadi ya wanyama hao imepungua sana kutokana na kuharibiwa kwa maeneo wanamoishi, uwindaji haramu na migogoro ya kisiasa katika maeneo mengi Afrika.
Baadhi ya aina wa twiga, sana maeneo ya kusini ya Afrika, wanaongezeka hata hivyo.
Hadi kufikia sasa, IUCN hawakuwa wameorodhesha twiga kuwa miongoni mwa wanyama walio hatarini.
Hata hivyo, kwenye orodha yao mpya ya wanyama walio hatarini, mnyama huyo ameorodheshwa kuwa "hatarini", baada ya idadi ya wanyama hao kushuka kwa zaidi ya asilimia 30.
Kwa mujibu wa Dkt Julian Fennessy, mwenyekiti wa kundi la IUCN linaloshughulikia twiga, wanyama hao "wanaangamia kimya kimya."
"Ukienda kwenye safari, twiga wapo kila mahali," aliambia BBC News.
"Ingawa kumekuwepo na wasiwasi kuhusu ndovu na vifaru, twiga wamesahaulika. Ni jambo la kusikitisha kwamba idadi yao imeshuka sana na ni jambo la kushangaza, kwamba wamepungua hivyo katika kipindi kifupi."
Ongezeko kubwa la idadi ya watu limesababisha maeneo mengi ya misitu kuharibiwa kwa ajili ya kilimo, jambo ambalo limepunguza maeneo wanamoishi twiga.
Vita katika baadhi ya maeneo Afrika pia vimeathiri idadi yao.
"Katika maeneo haya yenye vita na migogoro, hasa kaskazini mwa Kenya, Somalia na Ethiopia katika mpaka wake na Sudan Kusini, twiga ambao ni wanyama wakubwa wanaliwa."

MTAALAMU WA KUBIKIRI VIBINTI KUMBE AFYA YAKE NOMAA... ALISHA BIKIRI ZAIDI YA 100...


Rais wa Malawi, Peter Mutharika juzi alitoa amri ya kukamatwa kwa Eric Aniva ambaye hivi karibuni alibainika kufanya kibarua cha kuwabikiri mabinti wa chini ya umri wa miaka 13 zaidi ya 100.

Amri hiyo ya Rais imekuja baada ya kubainika kuwa mwanamume huyo maarufu kwa jina la ‘Fisi’ anaishi na Virusi vya Ukimwi (VVU). 

Mutharika alisema lazima mwanamume huyo akamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi yake kwa kuwa, kwa makusudi alifanya vitendo viovu akijua anaishi na VVU na lengo lake lilikuwa kuwaambukiza mabinti hao.

Aniva aliingia matatani baada ya kukiri katika mahojiano akijinasibu kuwa anaendesha maisha kwa kuwabikiri mabinti na kwamba hulipwa kuanzia dola nne za Marekani mpaka saba ambayo ni wastani wa Sh10,000 kwa kila mtu.

Mwanamume huyo alisema wazazi wa mabinti huwa wanampa kibarua cha kuwavusha kutoka utoto kuingia katika utu uzima na kwamba hatua hiyo ni sawa na tambiko

WAKE WA MARAIS WENYE MVUTO ZAIDI AFRIKA... PICHA ZIKO HAPA...

Wake wengi wa Marais husifika kwa kuwa na muonekano mzuri mbele ya jamii inayowazunguuka na pia hutumia nafasi zao kuhakikisha wanakuwa katika mazingira mazuri na ya kuvutia wakati wote. na hii inasababishwa zaidi na title ya u first lady. neno hili huwafanya muda wote wawe katika muonekano wenye mvuto zaidi ili muonekano wao uendane na neno hilo.
Hii Hapa ni List ya wake 10 wa Marais wa Afrika wanaoongoza kwa mvuto zaidi
LADY1
1) Princess Lalla Salma (Morocco)
LADY2
2) Sylvia Bongo Ondimba (Gabon)
LADY3
3) Chantal Biya (Cameroon)
LADY4
4) Hinda Deby Itno (Chad)
LD5
5) Zeinab Suma Jammel (Gambia)
LD6
6) Queen Inkhosikati LaMbikiza (Swaziland)
LD7
7) Ana Paula dos Santos (Angola)
LD8
8) Olive Lembe di Sita Kabila (Democratic Republic of Congo)
photographe
9) Dominique Folloroux-Ouattara (Ivory Coast)
LD10
10) Margaret Gakuo Kenyatta (Kenya

DIAMOND... SASA NIKO TAYARI KWA KIFO...

diamond mtoto         Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mtoto wake Latifah ‘Princess Tiffah’.

SIKU chache baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kupata binti na kumwita Latifah ‘Princess Tiffah’ na kuanza maisha mapya ya familia na mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’, nyota huyo anadaiwa kutoa ya moyoni kwa kusema kuwa sasa yupo tayari kwa kifo kwa vile ndoto yake kubwa ya kupata mtoto imekamilika na ana chata duniani.


KWANZA ANAMSHUKURU MUNGU
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Diamond alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumtimizia ndoto yake ambayo amekuwa akiiota usiku na mchana na kwa miaka mingi tangu kuingia ‘ukubwani’ hivyo, bahati mbaya yoyote ikitokea akapoteza uhai itakuwa poa tu kwake.
NDICHO KITU ALICHOBAKIZA
Chanzo kilikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa kuhusu mafanikio ya kimuziki na kimaisha, nyota huyo anaamini alishafikia malengo, alibakiza kimoja tu, mtoto.
“Unajua katika maisha, ukipata mali au mafanikio mengine ujue tatizo kubwa litabaki kwenye familia na familia yenyewe si kupata mke au mume bali kupata mtoto.
“Sasa jamaa siku zote alikuwa akisema, pesa kwake si tatizo, nyumba ya kuishi nzuri anayo, gari la kutembelea pia. Kilichokuwa kikiuchakaza moyo wake ni kutopata mtoto ili awe kama wengine. Hicho ndicho kitu alichokuwa amebakiza hapa duniani,” kilisema chanzo.
ZARI NAYE HANA FURAHA YA MTOTO
Chanzo kikazidi kudai kuwa, wakati Diamond akifurika machozi ya furaha kwa kupata mtoto, mzazi mwenziye, Zari yeye hana furaha kufuatia baba wa watoto wake watatu au aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga kumpiga madongo kupitia mtandao wake wa Instagram.
Mfano, juzi kwenye mtandao wake, jamaa huyo ametupia picha akiwa na mtu anayedaiwa kuwa eti, ndiye baba wa mtoto Tiffah.
“Zari anaujua ukweli kwamba mtoto ni wa Diamond. Sasa wale jamaa kuendelea kutangaza si wa Diamond wao wanajuaje wakati siri ya mtoto ni wa nani anaijua mama? Hayo ndiyo maneno ya Zari kila kukicha.
“Yeye ni mtu mzima, ana akili timamu. Hawezi mtoto wa huyu akampa yule. Nadhani maneno ya aliyekuwa mumewe ndiyo yanamkosesha raha. Lakini Diamond mwenyewe ni peace tu.” Chanzo.
Baada ya kujazwa ubuyu huo, paparazi wetu alifanikiwa kukutana uso kwa macho na Diamond mwenyewe ambaye kweli alionekana mwenye furaha muda wote na hata alipogusiwa hilo alimshukuru Mungu akisema maombi yake yamekubaliwa.
STUDIO YA DIAMOND HAIKALIKI
Habari zaidi zinasema kuwa, nyota huyo kupata mtoto imekuwa ‘nongwa, watu hawali wala hawanywi’. Hapatikani kwenye studio yake ya Wasafi Record iliyopo Sinza Mapambano.
Amani lilifika juzi na kumkosa lakini mmoja wa wafanyakazi wake alisema: “Weee! Chezea kichanga wewe. Baba Tiffah anakuja lakini si kama zamani. Unajua kwa sasa muda mwingi yupo na mwanaye.”
MSIKILIZE
Baadaye Amani lilimpata Diamond kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alisema: “Kusema kweli namshukuru Mungu kwa kila jambo ila zaidi kunipatia huyu Princess Tiffah. Kwani uwepo wake ni furaha kwangu na ni historia kubwa katika maisha yangu.
“Leo hii ikitokea nikafa basi watu watanikumbuka zaidi wakimuona mwanangu, maana huyo ndiye mrithi wa kila kitu kwangu.“Nilikuwa najiuliza nikifa sina mtoto itakuaje? Ina maana sitaacha kumbukumbu. Lakini kwa sasa nipo tayari kwa kifo kama Mungu amenia-ndikia

JOKATE AMFUNGUKIA DIAMOND KINAGAUBAGA... SHUKA NAYO HAPA...

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Jino kwa jino! Sexy lady anayefanya poa na ngoma yake ya Leo Leo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, amemlipua aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye hivi karibuni alimwita makombo baada ya kusikia kwa sasa anatoka kimalovee na msanii Ali Kiba.
 
Akizungumza na nasi wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata yeye ni makombo na bado anakula makombo?
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
“Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia kuwa ninatoka  au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii.
“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond na kuongeza:
“Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya msingi ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na hiyo.”

MAPYA KUHUSU WEMA SEPETU... ILI AZAE ANATAKIWA KULALA JUU YA KABURI... KANUMBA AHUSIKA... SOMA KISA...

Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.

Waandishi wetu
Mshangao! Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa ili azae, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya kaburi.
Hayo yanakuja siku chache baada ya Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo mzee huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.

Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba.
Akizungumza na waandishi wetu, baba huyo alisema kama kweli Wema alitoa mimba ya Kanumba basi atakuwa alijilaani kwa sababu ukoo wao ukitoa mimba unaweza kufa au kujilaani (kutokupata mtoto) hivyo anatakiwa kutambika kwa kulala juu ya kaburi la mama mkubwa wa Kanumba ambaye ni bibi wa babu wa mzee Kanumba.
Alisema sambamba na hilo, Wema atatakiwa kurithiwa na ndugu wa Kanumba (kati ya kaka au mdogo wake).
“Kwenye ukoo wetu ukitoa mimba kuna mambo mawili, moja ni kufariki dunia au ‘kujikila’ (kujilaani) kwa kutokuzaa, pengine ndicho kilichomtokea Wema,’’ alisema baba Kanumba.

KUTAMBIKA KABURINI
Mzee huyo alisema kuwa mama mkubwa huyo alishafariki dunia kwa hiyo yeye na marehemu Kanumba walipaswa kwenda kaburini kwake kufanya tambiko zito, wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kiasili na mikononi wameshika vibuyu, jambo ambalo lingempasa Wema kukaza moyo.Alisema kuwa wakiwa kaburini hapo, Wema alitakiwa achotewe mchanga na kushikishwa kisha kusemewa maneno ya kuomba msamaha kwa kilichotokea.

VITU VYA TAMBIKO
Alisema walitakiwa waende na maziwa, unga wa mtama na hayo mavazi maalumu kwa ajili ya tambiko hilo.

KURITHIWA NA NDUGU
Aliendelea kudadavua kwamba, kwa sasa Kanumba hayupo duniani hivyo Wema anapaswa kuchukuliwa na kaka au mdogo wake wa damu kwenda kutambika, ikiwa ni pamoja na kuzaa naye ili kufungua mlango wa kizazi, hata kama ataachika basi ataendelea kupata watoto.

MAMA MKUBWA NI NANI?
Baba Kanumba alisema mama mkubwa huyo ni bibi yake mzee Charles Kanumba ambaye katika ukoo wao alikuwa mganga wa wanawake walioshindwa kupata watoto au wenye tatizo la kizazi.

Hata hivyo, baba Kanumba alimalizia kwa kusema kuwa, ingekuwa zamani ilikuwa ni kurithiwa tu lakini kwa sasa mila hizo zinapingwa vikali.Gazeti hili lilipomtafuta Wema ili kumfikishia taarifa hizo hakupatikana hivyo jitihada zinaendelea.

KWA WANAWAKE... ZIJUE DALILI ZA MPEZI AKIWA ALIYEFULIA KI PESA...

MW 

Labda inawezekana unazijua dalili chache za Mwanaume aliyefulia lakini kuna nyingine za ziada kutoka kwa Mike Tee, ukishazisoma hizi niambie unakubaliana nayo kwa asilimia ngapi au dalili zipi hapa umeshawahi kukutana nazo?

MIKE TEE MAY 13 2015 DALILI ZA MWANAUME ALIYEFULIA

YALIYOJIRI MAADHIMISHO YA MUUNGANO TANZANIA

Rais Dk. Jakaya Kikwete na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa katika maadhimisho ya muungano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.

VURUGU ZATOKE BURUNDI... HATUMTAKI RAIS NKURUNZIZA...

Waandamanaji wakiwa Mjini Bujumbura.
Kumezuka ghasia katika Mji wa Bujumbura nchini Burundi kati ya maofisa wa polisi na waandamanaji wanaoishutumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba.
Waandamanaji walirusha mawe na kuchoma matairi huku maofisa wa polisi wakilazimika kurusha mabomu ya machozi hewani.
Ghasia hizo zinafuatia tangazo la jana kwamba Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwania muhula wa tatu wa urais.
Upinzani umeitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa katiba na kuonya kuwa huenda ikaathiri makubuliano ya amani ambayo yalimaliza miaka kadhaa ya mapigano ya kikabila.
Serikali imesema kuwa maandamano hayo si halali.
Maelfu ya raia wa Burundi wamelitoroka taifa hilo katika majuma ya hivi karibuni wakihofia kuongezeka kwa ghasia hizo huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi utakaofanyika Mwezi Juni mwaka huu.

BOFYA LIKE KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA

TAZAMA PICHA ZA MAZISHI YA BABA WA P SQUARE... ALIZIKWA JANA JAN. 30. 2015

Psq VIIMzee Moses Okoye, baba mzazi wa mastaa wa muziki kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye wa kundia la ‘P Square’ alifariki November 25 2014 baada ya kuanguka kwenye ngazi ndani ya nyumba.
Taarifa za wanafamilia zilisema mzee huyo alifanyiwa upasuaji wa goti siku za nyuma na hali yake ilianza kuwa sawa kabla ya kufariki ambapo leo January 30, 2015 ndio mzee huyu amezikwa ikiwa ni miaka miwili imepita toka kufariki kwa mama yao.
Hizi ni picha za safari ya mwisho ya Mzee Moses Okoye, baba wa mastaa mzazi wa P Square na Jude ‘Engees’ Okoye.
Ps
Psq II
PSq Iv
Psq IX
.
Peter na Paul Okoye.
Psq VI
PSQ vkas
.
Peter na kaka yake Jude Okoye.
pSQ
P S 1
PS 2
PS 3
Kulikua na ulinzi pia
Kulikua na ulinzi pia
ps 5
ps 6
Endelea kufuatilia modesigntz beste wangu wa ukweli, nami ntaendelea kukupa kila habari inayonifikia... pia usisahau kulike page yetu ya facebook andika modesign the like...na usikose kunifollow instagram kama modesigntz nami ntakufollow back...
© Copyright MO Design
Back To Top