MWANAMUZIKI Iyanya aka ‘Mr Oreo’ wa Nigeria, amekolea katika penzi la muigizaji rembo ambaye ni chipukizi anayeshiriki naye katika maandalizi ya filamu iitwayo ‘Superstar’.
Filamu hiyo ambayo inadhaminiwa na raia wa Nigeria anayeishi Marekani, Tony Abulu, itahusisha pia wasanii maarufu ambao ni: Tekno, Jide Kosoko, Tina Amuziam, Rachael Oniga, Funnybone, Pencil, Bryan Okwara, Lilian Esoro na wengine.
Abulu, ambaye amekuwa katika tasnia ya burudani kwa zaidi ya miaka 30, amekamia kuitangaza zaidi tasnia ya muziki wa Nigeria duniani ili kuipa umaarufu kama wa tasnia ya filamu ya Nigeria ambayo hujulikana kama Nollywood.
Filamu nyingine za Abulu katika tasnia hiyo ni pamoja na ‘Doctor Bello’, ‘Back To Africa’ na ‘Crazy Like a Fox’.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.