Imelda mtema
UBAVU wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amefunguka kuwa atapiga picha moja ya utupu ili kuwakata vilimi wanaopenda kumzungumzia vibaya.
Zari ametoa kauli hiyo hivi karibuni kufuatia wafuasi wa Mtandao wa Instagram kumnanga kuwa hakutumia busara kuposti picha zake za nusu utupu akiwa mjamzito.
Alisema kwa kuwa watu wameshindwa kumuelewa kipindi hicho, wakati ujao atapiga picha za utupu ili wamuone vizuri kama alivyofanya mwanamuziki wa Marekani, Kimberly Kardashian ‘Kim Kardashian’.
“Nitapiga ya utupu kabisa ili muone nikiwa mjamzito. Uzuri ni kwamba baba T (Diamond) ameshafikiria kuhusu kutafuta mdogo wa Princess Tiffah (mtoto wa Diamond),” aliandika Zari katika mtandao wake wa Instagram huku akitupia picha ya utupu ya Kim Kardashian akiwa mjamzito
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.