Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ZARI AMFUNGUKIA DIAMOND PLATNUMZ LIVE BILA CHENGA

ZALI & DIAMOND

ZARI The Boss Lady; ni baby mama wa supastaa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz anayeiwakilisha vyema Tanzania ambaye ametema nyongo kwa kumchamba jamaa huyo laivu bila chenga.

Ikumbukwe kwamba, Zari; raia wa Uganda anayeishi nchini Afrika Kusini amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi ambao ni Tiffah Dangote na Prince Nillan.

 

Katika sehemu ya pili ya shoo yao ya Young, Famous and African inayoendelea kwenye jukwaa la Netflix katika Mtandao wa YouTube, Zari anapiga stori na mwigizaji Khanyi Mbau wa Afrika Kusini ambapo anamueleza kwamba aliona ni bora alee watoto wake mwenyewe kuliko kuwa na kinyongo na Diamond ambaye alimsaliti mara nyingi mno.

 

Mwishoni mwa sehemu hiyo ya pili ya shoo hiyo ndipo hapo Zari akawa uso kwa uso na Diamond ambapo anamchamba laivu akifunguka yote mazito ambayo hajawahi kufunguka.

 

Zari anamwambia Diamond kuwa aliwahi kuwaza kuwa na familia yake; kwa maana awe na Zari kama mke hapa na watoto wake hapa?

Hapo Diamond hakuwa na majibu na kumfanya Zari kuendelea kumpa somo kwamba alimkatia tamaa na kumfanya jamaa huyo atulie tuli!

 

Zari anamwambia Diamond: “Unaona ulivyojishusha kama hapa, hukuwahi kujishusha wakati ule tukiwa pamoja, ulikuwa unapanda juu sana, ulijiona staa mkubwa, lakini nadhani leo umeelewa ni hasara kiasi gani umesababisha.”
Zari anaendelea; “Nilikuwa na uwezo wa kupigwa risasi kwa sababu yako kwa jinsi ambavyo nilikuwa ninakupenda.
“Mimi na watoto tulikuwa tunashambuliwa Baba Tee (Diamond), tulikuwa tumechoka, hukutulinda, hukufanya chochote.”

 

Wakati wote huo Zari akiwa anafoka kwa hisia kali na kulengwalengwa na machozi, Diamond alikuwa anatazama pembeni na kujigeuza asijue nini cha kujibu kwa namna alivyomuumiza kutokana na usaliti aliomfanyia kiasi cha kuzaa nje ya uhusiano wake ambapo alizaa na Hamisa Mobeto.

 

Itoshe kusema kuwa, kwenye shoo hii, hasa sehemu hii ya pili, Zari amemtolea uvivu Diamond na kutoa kile kilichoukamata moyo wake juu ya mzazi mwenzake huyo, jambo ambalo hakupata kulifanya.
Kwa kufanya hivyo, wengi wanaamini kuwa, Zari atakuwa ametoa kitu kikubwa na sasa roho yake itakuwa kwatu kabisa.

WEMA AMCHANA LIVE HARMORAPA MTANDAONI...



MSANII wa filamu nchini Wema Sepetu, ‘Madam’,  ambaye hivi karibuni alihamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amefunguka baada ya Msanii wa Bongo Fleva, Harmorapa kujinadi mtandaoni kuwa yupo tayari kumuoa Wema.

Wema amefunguka na kuandika kuwa anamheshimu Harmorapa kama msanii mwenzie hivyo kitendo cha kujinadi mtandaoni kuwa yupo tayari kuwa na Wema katika mahusiano si sawa ajaribu kwa watu wengine na si yeye.
Aidha Wema ameandika kuwa kitendo cha Harmorapa kujinadi ni kumchafulia heshima yake kwa jamii na kwa chama chake cha CHADEMA.

ALICHOKISEMA NAY WAMITEGO BAADA YA KUKAMBATWA NA POLISI...



MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva anayefanya sanaa yake tofauti na wasanii wengine, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego‘ inadaiwa amekamatwa na polisi mkoani Morogoro akiwa Hotelini mara tu baada ya kumaliza kazi zake zilizompeleka huko.

Msanii huyo amekuwa akiimba nyimbo zenye tungo tata na inadaiwa huwenda amekamatwa kwa ajili ya kutumbuiza wimbo wake mpya uitwao ‘Wapo’, unaoendelea kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.






E. MBASHA NA JACQUELINE MAPENZI MUBASHARA... FLORA MBASHA KULEE...



Baada ya kuficha uhusiano wao, Mwimbaji wa Gospo Bongo, Emmanuel Mbasha na Mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa, sasa siyo siri tena kwani mambo yako hazarani sasa. Mtu aliyevujisha picha zao za kimahaba, akisema kuwa, Mbasha na Jack kwa sasa hawajifichi tena kwani wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali kama kanisani, sehemu za starehe na hivi karibuni walikuwa wakijiachia Siku ya Wapendanao huku wakiwa kwenye mavazi rasmi ya wapenzi.

“Naona wameamua kuweka mambo mubashara kabisa kwa sababu Mbasha ameshasarenda kwa aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha maana sasa ni malavu kwa kwenda mbele. Ukikutana nao hata hawajifichi ,”



kilimwaga ubuyu chanzo chetu. Baada ya kupata ubuyu na picha hizo kutoka kwa sosi, mwanahabari wetu alimwendea hewani Jack ambaye muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania mkoani Kilimanjaro ambapo alifunguka kuwa, hapendi kuzungumzia kiundani mambo yake ya uhusiano lakini anachojua ni kwamba, yeye na Mbasha ni marafiki na muda ukifika, kama kuna kinachoendelea ataweka wazi kila kitu. “Muda ukifika nitaweka wazi kila kitu kama kuna mambo ya ndoa na uchumba, wala msiwe na wasiwasi ninyi mtaona tu, suala hilo huwa halina kificho,” alisema Jack kwa bashasha.

Alipotafutwa Mbasha simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu pamoja na kwamba ulionesha kupokelewa.

ALIYEKUWA MPENZI WA WEMA AFUNGUKA HAYA MAZITO...



MCHEKESHAJI maarufu Bongo na aliyekuwa mshiriki wa shindano na ‘Big Brother Africa’, Idris Sultan amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa sauti ya Wema ilirekodiwa bila ya Wema mwenyewe kujua. Idris amefunguka kwa wanaokwenda kumtembelea Wema wengi ni wanafiki na wanamalengo yao mengine tofauti na kwenda kumjulia hali Wema.


Mpaka hivi sasa sakata hili bado linaendelea kupata sura mpya na kuwa gumzo zaidi nchini.
“Na muendelee kupiga kulele kutembelea watu central na recording people bila wao kujua. Kwakua tunachukulia maisha ya watu kama mfumo wa likes na following bila kujua tunawaumiza kiasi gani kwa tunachokifanya basi let us proceed na tutaona kama tunaowapenda kama tunavyosema tutakua tumewatendea haki. Kwa hili nimeshindwa kunyamaza you claim to be friends and true people kumbe unafiki unatujaa. We will kill our families and be the 1st to cry kwenye Msiba WHERE IS HUMANITY? kama hamjapenda kutoa moral support basi kaeni majumbani kwenu na mposti posti vimachozi na unafiki wenu sio hata pale pasafi padogo palipo baki” Aliandika Idris 

MANARA WA SIMBA SC. KUMPOSA MLIMBWENDE WEMA SEPETU...

Haji Manara (Kushoto), Wema Sepetu (Kulia).
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amelipa mtihani mwingine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuahidi kufanya maamuzi makubwa endapo ratiba ya ligi kuu haitabadilishwa hadi mwisho wa msimu.
Maamuzi ambayo Haji ametangaza kuyafanya ni kumposa mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 Wema Sepetu na kumuoa endapo atakubali, lakini kama hatakubali, Haji ameahidi kutembea akiwa amevaa nguo ya ndani pekee (Boxer) kutoka nyumbani kwake hadi katika ofisi za TFF zilizoko Ilala Dar es Salaam.
“Nimalizie Kwa kuwapa mtihani mwingine TFF na bodi ya Ligi, iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe la shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka Nyumbani kwangu hadi TFF” Amesema Manara
Hatua hii ya Haji imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo kati ya Simba na Yanga uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 18, mwaka huu na sasa utachezwa Februari 25 mwaka huu.
Hatua hiyo ya Bodi ya Ligi imekuja kama kutimiza kile ambacho Manara alikiahidi awali mwanzoni mwa msimu, ambapo alisema kuwa angetembea akiwa mtupu endapo ratiba ya ligi isingebadilishwa.
Katika tamko lake la sasa kupitia ukurasa wake wa Facebook, Manara ameeleza kusikitishwa kwake na kile alichokiita ubabaishaji katika upangaji ratiba, na kulitaja suala hilo kuwa ni moja ya sababu ya Tanzania kukwama katika soka.
“Ninajiuliza iwapo ratiba ya Ligi yetu ni muhali kuipanga, vipi kuhusu program nyingine za maendeleo? Itakuwaje kuhusu timu yetu ya taifa juu ya ndoto zetu za mchana wa jua kali? vipi kuhusiana na zile programu hewa za soka la vijana, watoto na wanawake?”
Ameendelea kusema “Hakika kwetu hayo ni sawa na bahari ya Mediterranean au bahari kuu ya hadithi za Alfu Leila uleila, hatuwezi ratiba tutaweza kwenda Afcon 2019? hatuwezi kupanga ratiba tutaweza kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza mchezo huu ambao yatajwa watu bilioni tatu duniani kote wanaushabikia?”

NI MIEZI MITANO TU LAKINI HII HAPA NYUMBA NA GARI LAKE... RAYMOND...

Ni mwimbaji mwingine staa wa bongo fleva, makofi mengi amepigiwa kwenye utunzi pamoja na ukali wa melody, anaitwa Rayvanny kutoka WCB ambaye ngoma yake ya kwanza kuiachia toka yuko chini ya lebo ya WCB aliiachia ‘kwetu‘ April 2016.
Anazo sifa nyingine za uchapakazi pia na ndio maana leo anafurahia mafanikio/hatua yake kwa kipindi hiko kifupi ambapo aliweka picha ya nyumba na gari lake na kuandika ‘Daaah eti na mimi leo naingia kwangu, kweli Mungu hana upendeleo (swala la nyumba na gari mimi………. )
screen-shot-2016-09-17-at-11-51-37-am
screen-shot-2016-09-17-at-11-51-50-am

IKO HAPA KAULI YA NUH MZIWANDA KUHUSU KURUDIANA NA SHILOLE...


Staa wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii kabisa kurudiana na mwanadada huyo.
Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana.

Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake wa zamani Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
“Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana.
Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema Nuh

WEMA KUMBURUZA DIAMOND MAHAKAMANI KISA KIKO HAPA... IKO HAPA NA VIDEO YA NATAFUTA KIKI...


Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu anaandaa utaratibu wa kumfikisha mahakamani aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia kitendo cha msanii wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Raymond ‘Rayvanny’ kumtumia kwenye video ya wimbo wake wa Natafuta Kiki bila makubaliano. 

Msanii wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Raymond ‘Rayvanny’.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Wema alisema amefikia uamuzi huo kutokana na Diamond kukiuka makubaliano waliyofanya awali kuhusu yeye kuonekana kwenye video hiyo. Alisema: “Diamond alinifuata na kunitaka nionekane kwenye video ya msanii wake Raymond, nikamwambia anipe milioni 10, yeye akaonesha alikuwa anataka free huku akisema mbona nilimsaidia Ommy Dimpoz.

Rais Wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’,  Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Nilimwambia kuwa nilimsaidia Dimpoz kwa kuwa alikuwa anahitaji msaada lakini yeye nilitaka anipe kiasi hicho cha pesa. “Baadaye niliongea na Martin Kadinda kuhusu kile alichotaka Diamond na pesa ambayo nilimtajia, Martin akaniambia kwa ishu hiyo hata milioni 10 ni ndogo, nikashituka na ndiyo maana hata Diamond aliponipigia tena kuhusu ishu hiyo nilimchomolea.” Wema akaendelea kudai kuwa, licha ya kwamba yeye alishakataa kuonekana kwenye video hiyo, siku ya ‘bethidei’ ya Rommy Jones alifanyiwa kitendo ambacho si cha haki.

 Kipande cha video kilichotumika  kwenye video ya wimbo wa Natafuta Kiki bila makubaliano.
“Nikiwa pale kwenye ‘bethidei’ ya Rommy, bila kujua wana lao jambo, Raymond akawa anajiweka sana kwangu huku video na picha mbalimbali zikichukuliwa, sikujua kwamba kuna kitu nyuma yake, ile video ilipotoka nikashangaa nimetumika bila ridhaa yangu.
 “Ndiyo maana nimewasiliana na wanasheria wangu ili nimshitaki Diamond kwani yeye ndiye niliyezungumza naye na tukashindwana,” alisema Wema. Kufuatia tuhuma hizo, Risasi lilifanya jitihada za kuwatafuta Diamond na Raymond  ili kuzungumzia madai hayo lakini hawakuweza kupatikana mara moja. Alipotafutwa meneja wa Diamond, Salam Sharraf alisema: “Mimi sidhani kama kuna ishu hapo maana hata baada ya ile ‘bethidei’ ya Rommy, Wema aliiposti ile video kwenye ukurasa wake wa Insta kuonesha kuwa hakuwa na shida na sisi tukajua hata kwenye kuonekana kwenye ile video si tatizo.”

IKO HAPA VIDEO YA MIJI WALIYOKULIA MESSI, RONALDO,AGUERO, NEYMAR NA WENGINEO

Alhamisi ya August 18 2016 naomba nikuletee video ya miji waliokulia mastaa 15 wa dunia ambao wengi wetu tumezoea kuwaona katika mafanikio yao katika vilabu vya Ulaya.
Leo naomba nikuletee miji ya mastaa wa soka kama Lionel Messi aliyezaliwa Rosario Argentina, Zlatan Ibrahimovic aliyekulia Malmo Sweden, wengi wao tumewahi kusikia historia zao kuwa hawakutokea katika familia zenye maisha mazuri ila video inaonesha mitaa yao ilivyokuwa kwa sasa na baadhi zamani pia

MATITI YA KAJALA MH... CHAINIZI WAHUSISHWA...

tatu
Baada ya gumzo kubwa kuibuka juu ya muonekano mpya wa matiti ya msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja, shostito wake wa karibu amemwaga ubuyu kuwa, dawa za kuongeza matiti za Kichina zinahusika.
Akipigia stori hivi karibuni, mtoa ubuyu wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, huko nyuma matiti ya Kajala yalikuwa ‘ndala’ akawa anatumia dawa f’lani za kupaka ili kuyafanya yatune.
“Nyie muoneni vile tu lakini zile nido zake za sasa Mchina anahusika sana, hawezi kuanika ukweli lakini habari ndiyo hiyo,” alisema mtoa ubuyu huyo.
Paparazi wetu alibahatika kuongea na Kajala juu ya madai hayo ambapo alisema: “Watu bwana wanaongea sana, je nikiamua sasa kutumia hizo dawa itakuwaje? Niseme tu kwamba matiti yangu ni orijino na siku zote yana mvuto ndiyo maana sionagi hatari kuyaanika.

NI BALAA ... IKO HAPA HII YA PICHA ZA MALOVEE KUMFIKIA BWANA HARUSI HONEY MOON


MAPICHAZ (1)Mwanamke huyo akijiachia ‘kimalovee’ na boyfriend wake wa zamani.

DUNIA ina maajabu! Mwanamke mmoja (jina halijajulikana mara moja) amejikuta akivunja ndoa yake ya wiki moja baada ya picha zake za utupu akijiachia ‘kimalovee’ na boyfriend wake wa zamani kumfikia mume wake wa ndoa wakati wakiwa fungate (honey-moon) baada ya ndoa yake na mumewe iliyofanyika jijini Dar es Saalam.
Tukio hilo la aibu limetokea wiki moja tu baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha. Kupitia ujumbe wa sauti mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo alijipiga na mpenzi wake zamani miaka saba iliyopita wakiwa chuoni.

MAPICHAZ (2)Akiongea kwenye Ripoti ya Siku ya kipindi cha Ubaoni cha EFM , mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo zimedhamlilisha mno kiasi cha kuiharibu ndoa yake, kuwaumiza ndugu zake na kuwakosea heshima wakwe zake na kwamba anajuta kupita kiasi.
“Ni kweli ni mimi ndiye niliyepiga hizo picha lakini ni muda mrefu tangu kipindi nikiwa chuo, yaani hata huyo mtu mwenyewe sijui yuko wapi sina mawasiliano naye tena, sikutegemea kiukweli,” anasema mwanamke huyo.

ongeza“Ni kitu ambacho kinaniuma na kimeniharibia mlolongo mzima wa maisha yangu, mpaka sasa hivi sielewi, mume wangu hawezi kunielewa tena na yeye ndio nimemwekea kama nguzo, ndio kila kitu kwasababu hata familia yangu hainielewi ,” ameongeza.
“Mpaka sasa hivi sijui nafanya nini.”
Kwa upande wa mume wake, alidai kuwa picha hizo zimeuvunja moyo wake.
“Tulikuwa tumeshaenda kwenye honey moon tumerudi, sikuamini macho yangu baada ya kuona hizo picha na huyu mwanamke, rafiki zangu walikuwepo wengi sana, best man wangu pia ni vitu ambavyo kuvizungumza mimi nashindwa, naanzia wapi, lakini mapenzi huwa yako hivyo, inawezekana iko hivyo lakini sasa kama mazingira kama yale hata kama ukiwa ni wewe lazima utaumia, familia yangu ntaiambia nini mimi, imenigharamia harusi kubwa,” alisema mwanaume huyo.
Amedai kuwa haoni kama inawezekana tena kukaa chini na mke wake huyo kwa kile kilichotokea.
“Nikae chini ili iweje?” alihoji kwa jazba. “Imeniuma, imeniumiza sana hii kitu haki ya Mungu, hata kama miaka kumi imepita kwanini imekuja kwenye harusi yangu, zawadi zimekuja kwaajili ya harusi yetu kwanini aletewe picha za aina hiyo? Angeniambia before kwamba nilikuwa na moja mbili, ningekuwa najua, lakini amenificha. Imenicost kwa kiasi kikubwa sana, nitaiambiaje familia yangu kwa mfano? Nitasema nini.”
“Sitokuja kupenda tena mwanamke wa aina yoyote ile, mpaka nakuja kuingia kaburini, I swear to God, imetosha kabisa.”
Wawili hao walifunga ndoa tarehe April 23 mwaka huu.
Sikiliza maelezo kamili ya mwanamke huyo hapo chini

BARAKA DA PRINCE AFUNGUKIA SAKATA LA KUMZALILISHA LIHAH... NAJMA AHUSISHWA...


Barakah da Prince na mpenzi wake, Naj.
Juzikati wasanii Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ na Estelina Sanga ‘‘Linah’ walinaswa wakiwa kimahaba, tukio lililoibua gumzo na wengi kudhani mkali huyo wa ngoma ya Siwezi tayari kachepukia kwa ndege mnana.
Barakah da Prince na Linah.
Baraka na Linah walinaswa katika viunga vya Escape One kulikokuwa na shoo ya Christian Bella ambapo jamaa alionekana akimshikashika mdada huyo bila aibu.
Akilifungukia tukio hilo, Baraka alisema kuwa, yalikuwa ni mapozi ya kawaida tu na wala watu wasihisi anachepuka na Linah.
“Hivi nimsaliti Naj (Najma mpenzi wake wa sasa) sijipendi? Yale ni mapozi ya kawaida tu. Narudia tena, nampenda sana Naj na hakuna mbadala wake,” alisema Baraka.

IKO HAPA YA BARAKA DA PRINCE KUMCHEZEA LINAH NYETI HADHARANI...


Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’ na Linah.
DAR ES SALAAM: Katika hali isiyo ya kawaida, staa wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’ amenaswa akimdhalilisha staa mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kwa kumshika sehemu zake nyeti.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita katika Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na shoo ya kuadhimisha miaka kumi ya staa wa Muziki wa Dansi, Christian Bella ‘Obama’.
Baraka na Linah waliokuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye ratiba ya kuburudisha siku hiyo, walifanya tukio hilo walipokuwa nyuma ya jukwaa (back stage) walipokuwa wakisubiri muda wao wa kutumbuiza ufike.
Paparazi wetu aliyekuwa akifanya ziara ya kushtukiza mara kwa mara back stage, kuna wakati alifanikiwa kumkuta Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa ushirikiano.
“Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.
Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Baraka, Linah alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.
“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.
Kwa upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.
Linah na Baraka waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake hadi waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA DIAMOND PLATNUMZ... MENO YA DHAHABU...

Unapokuwa na pesa unaweza kufanya kila kitu ukipendacho na kwa wakati uupendao, bila kujali jamii itazungumza nini kuhusu nini unafanya, ili mradi pesa zako zimekutuma kufanya kile ambacho toho yako imependa ukifanye.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz sasa anamuonekano mpya, na hii yote ni jeuri ya pesa yake anayoimiliki. mtu anaweza kusema ni muonekano mbata lakini ni wenye thamani kubwa.
ukimuangalia mdomoni utaona hayo mabadiliko ambapo sasa meno yake karibia yote ya chini ni dhahabu tupu.
Lakini pia Kupitia Twitter yake Diamond aliandika kuhusu ngoma itayowakutanisha wakali wawili ambao ni Harmonize wa Tanzania na Korede wa Nigeria.

IKO HAPA SABABU YA SIWEMA WA NAY WA MITEGO KUTOKA JELA... NAY AHUSIKA...


Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Siwema Edson.
HABARI njema! Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kutishia kwa njia ya mtandao, hatimaye ametoka jela.
Akipiga stori DSM, Nay wa Mitego alisema katika harakati za kushughulikia ili mzazi mwenzake huyo atoke alifanikiwa kupata mawakili wawili ambao mpaka Jumamosi iliyopita walifanikisha zoezi la Siwema kutoka na sasa atatumikia kifungo cha nje.
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake,  Siwema Edson
Nay wa Mitego alisema alilazimika kupambana kwa nguvu zote si kwa sababu anataka kuwa naye isipokuwa kama mzazi hakujisikia vizuri kuona mama wa mwanaye yuko jela wakati yeye anao uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya kumsaidia.
“Kulikuwa kuna njia mbili za kufanya, kukata rufaa au kubadilishiwa kifungo, mawakili wangu waliniambia niwaachie wao watamaliza.
“Hivi ninavyoongea na wewe niko mbali na mjini lakini taarifa za Siwema kutoka jela ninazo, kwa hiyo sina maelezo mengine zaidi ya hayo ila namshukuru Mungu kwa kulifanikisha hili,” alisema.
 Aprili mwaka huu Siwema alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa kosa la kutoa vitisho kwa kutumia mtandao.
Siwema na Nay walikuwa ni wapenzi wa muda mrefu ambapo walifanikiwa kupata mtoto mmoja lakini akiwa bado mchanga, Nay alimfumania mzazi mwenzake huyo na mwanaume mwingine na hivyo kuvunja uhusiano wao  huku akimchukua mwanaye huyo ambaye kwa sasa analelewa na mama wa Nay.

SHILOLE AFUNGUKA... ATOA SIRI 4 ZINAZOFANYA ATOKE NA VISERENGETI BOY...


Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na aliyekuwa mpenzi wake, Nuh Mziwanda

MSANII nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, baada ya kusemwa kwa muda mrefu, hatimaye amefunguka na kutoa sababu nne za yeye kupenda kutoka na wanaume wanaotajwa kuwa ni wadogo kwake kiumri.
Akizungumza na jijini DSM nyota huyo ambaye pia hufahamika kama Shishi Baby, alisema maneno ya watu juu ya jambo hilo siyo sahihi, kwani historia ya maisha aliyopitia ndiyo inayomfanya aonekane mkubwa, wakati yeye ni binti mdogo aliyezaa mapema.
Aidha, mkali huyo wa kibao cha Paka la Baa, alisema yeye hivi sasa ana umri wa miaka 30, ‘size’ kabisa kwa wanaume anaotoka nao kimapenzi, kwani hata hao nao, siyo watoto ‘kihiiivyo’ kama maneno ya watu yanavyosema.
Sababu nyingine ni;
Shilole na Nedy Music.
1: KUOGOPA KUZEESHWA
“Mimi ni kijana kutembea na wazee siwezi, naweza kujikuta nimezeeshwa bure kitu ambacho sikitaki hata kukisikia, kwani naamini bado nina uhitaji kama kijana.
“Angalia wasichana wengi wadogo wanaotoka kimapenzi na wazee hujikuta nao wanakuwa na mambo ya kizee, unadhani atafanya nini wakati ameshakubali kuzeeshwa?”
2: HATAKI KUBURUZWA
“Mimi napenda kuchakarika ndiyo maana sipendi kabisa penzi la wazee ambao ukiwa tegemezi kwao wanakuburuza. Wanawake wengi wanaotoka na wazee huwategemea kwa sababu ya uvivu wao wa kutafuta, kwangu mimi kazi tu!
3: ANASAKA PENZI LA KWELI
“Wasichana wengi wa mjini wamekuwa wakijiingiza kwa wazee lakini hawana mapenzi nao ya kweli, wanakwenda kuchuna pesa kisha wana viserengeti, mimi mwenzao nafuata penzi kwa hao vijana, wanajua kupenda na kwa sababu hobi yangu ni wao siwezi kuwa na wazee kwa kweli.”
4: VIJANA WANA NGUVU, WANAVUTIA
“Na uweke pia hii, kwamba vijana wana nguvu, damu changa na wanavutia, siwezi kutoka na wazee hawana mvuto.”
Baada ya kutaja sababu zake hizo, Shilole alihoji ni yupi mwenye afadhali kati yake na wasichana wenzake wanaotoka na wazee lakini wakiwa wavivu kutafuta?..
© Copyright MO Design
Back To Top