
Lionel Messi amefanikiwa kuvunja rekodi ya ufungaji wa muda wote katika timu ya taifa ya Argentina, amefunga jumla ya magoli 55 baada ya kufunga goli la dakika ya 32 katika ushindi wa magoli 4-0 nusu fainali ya Copa America 2016 dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo USA, awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na mkongwe Gabriel Batistuta.

Batistuta hadi anastaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina alikuwa kaifungia magoli 54, rekodi ambayo imevunjwa na Lionel Messi aliyefunga jumla ya magoli 55 na kuwa ndio mfungaji bora wa Argentina wa muda wote, magoli ya Argentina yalifungwa na Lavezzi dakika ya 4, Lionel Messi dakika ya 32 na Higuan dakika ya 50 na 86.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.