
Wengi walimtambua kwa jina la Mose P, wengine wakawa wanamwita Mo 7 au Mo P 7, aliwahi kutamba na ngomakama Harusi ya Kaka na Pamoja na Kadenti aliyoshirikiana na H Mbizo na Sniper wa Wakali kwanza.
lakini baada ya nyimbo hizo mbili alitoa album ambayo ilisambazwa na kampuni ya Mamu store iliyobeaba jina la Kifaranga cha Kuku enzi hizo, kisha akapotea kabisa na hakujulikana alikuwa anafanya nini.
Jina lake halisi ni Mussa Sikabwe, kwa wale walio karibu naye walijua alikuwa anafanya nini kwani kipindi hicho akifanya mziki alikuwa pia akisoma chuo cha uandishi wa habari.
kupotea kwake hakukuwa kupotea halisi kwani kuna vitu vingine vingi alikuwa anavifanya pia vinavyohusu muziki na video.
lakini ili kuwaonesha wale waliokuwa wanamfahamu kuwa hajapotea kabisa ameamua kuwaachia hii audio ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Kidonda ili watu wasiisahau sauti, na ujio rasmi utakuwa hapo baadae.
kwa sasa anatemmbelea jina la MO Design
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.