
wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa ambaye kwa sasa ni kocha wa Real Madrid
Zinadine Zidane.
Marco Materazzi ameweka wazi kilichomfanya Zidane ampige kichwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la dunia 2006, tofauti na ilivyokuwa inaripotiwa na wengi, Materrazi amekuwa akiombwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani lakini alikuwa akikwepa kuzungumzia suala hilo.

“Toka 2006 nimekuwa nikipokea maombi mengi ya kufanya interview, nimeamua kutoa kitabu kinachoeleza ukweli kwa sababu kila mtu anauliza ni nini nilimwambia Zidane hadi akapandwa na hasira na kunipiga kichwa, ni kweli maneno yangu yalikuwa ya kijinga lakini Zidane hakustahili kureact vile”

“Nimekuwa nikisikia vitu vingi kutoka katika miji jirani ya Rome, Naples, Turin, Milan Paris ila mimi nilimtusi kuhusu dada na sio mama yake kama nilivyosoma katika magazeti mengi, mama yangu alifariki nikiwa mdogo, hivyo nisingeweza kumtukania mama yake”
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.