Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

OBREY CHIRWA AWATISHIA NGOMA NA TAMBWE YANGA...



13450943_1178788475497017_9163122387765644343_n
Straika mpya wa Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia.

STRAIKA mpya wa Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia, ameendeleza kutishia uhai wa pacha ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe huku akisaka namba ya mmojawapo msimu ujao kutokana na uwezo mkubwa anaouonyesha kwenye mazoezi ya kikosi hicho.
Nyota huyo wa zamani wa FC Platinum ya Zimbabwe, jana aligeuka gumzo kwa mashabiki waliokuwa kwenye mazoezi ya Yanga baada ya kufunga bonge la bao la kichwa cha mkizi, kama alilowahi kufunga Robin van Persie wa Uholanzi katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Chirwa alifunga bao hilo kwenye mazoezi ya kikosi hicho yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, Dar ambako Yanga inajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, hatua ya makundi dhidi ya Medeama.
tulishuhudia Chirwa ‘akielea’ angani kuunganisha kwa kichwa krosi ya winga machachari, Simon Msuva katika mazoezi ambayo Kocha Hans van Der Pluijm aliigawa timu katika vikosi viwili.
Ajabu baada ya kuingia kwa bao hilo, mashabiki walilipuka kwa shangwe na kuanza kumshangilia huku wakisema: “Ngoma jiandae kwa moto huu wa Chirwa lazima kazi uwe nayo msimu ujao. Huyu jamaa ni noma aisee.
Bado kuna kitendawili cha nani aanze kwenye safu ya ushambuliaji kati ya Chirwa, Tambwe na Ngoma ambao kwa pamoja wamekuwa wakiwakosha mashabiki kwa ubora wao

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright 2025 MO Design | Designed By Code Nirvana