Jina la nahodha wa timu ya taifa ya England na klabu ya Man United Wayne Rooney linazidi kukaa kwenye vichwa vya habari kila kukicha, Rooney amerudi kwenye vichwa vya habari kwa mara nyingine tena baada ya mke wake Coleen Rooney kuoneshwa hisia zake za kusikitishwa kuzomewa mmewe katika mchezo dhidi ya Malta.
Rooney kwa sasa anaonekana kukutana na wakati mgumu katika soka lake baada ya kuonekana kuanza kukosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza chini ya kocha Jose Mourinho kwa mechi 3 zilizopita, kitendo cha kuzomewa kwa nahodha siku ya Jumamosi katika mchezo dhidi Malta Wembley hakikumfurahisha mkewe Coleen Rooney.
“Mechi kama ya kesho na una mtoto wa kiume ana miaka sita halafu awepo uwanjani anaangalia baba yake akizomewa, hilo sio sawa kiukweli” tweet hiyo imekuja jana yakiwa yameanza maneno ya kuwa Rooney atakosekana katika mchezo wa leo dhidi ya Slovenia.
KAMA HUJABAHATIKA KUSIKILIZA AU KUDOWNLOAD WIMBO WA MO DESIGN UITWAO KIDONDA BASI HUU HAPA
KAMA HUJABAHATIKA KUSIKILIZA AU KUDOWNLOAD WIMBO WA MO DESIGN UITWAO KIDONDA BASI HUU HAPA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.