Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

FAINI WALIOPIGWA MANCHESTER CITY NA CHELSEA IKO HAPA...

Chelsea wamepigwa faini ya £100,000 na Manchester City wakapigwa faini ya £35,000 baada ya wachezaji wao kuhusika katika vurugu uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya Premia.
Hisia zilipanda na wachezaji wakakabiliana mechi hiyo iliyochezewa uwanjani Etihad ilipokaribia kumalizika baada ya Sergio Aguero wa City kufukuzwa uwanjani kwa kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz.
Fernandinho pia alifukuzwa uwanjani kwa kumkaba koo Cesc Fabregas wachezaji wa klabu hizo mbili walipokabiliana baada ya kisa hicho.
Chelsea walishinda 3-1.
Blues walikuwa awali wametahadharishwa kwamba wanaweza kupokonywa alama kwa utovu wa nidhamu.
Viongozi hao wa Ligi ya Premia wamepigwa faini mara sita tangu Februari 2015 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji.
KAMA HUKUBAHATIKA KUONA VIDEO YA SAFARI YA CHEKA INDIA HII HAPA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top