Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

YAKO HAPA MATOKEO YA KIPIGO CHA ARSENAL NA TATHMINI YA MECHI

Arsenal wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Everton kutoka nyuma na kuondoka na ushindi wa 2-1.
Washika bunduki hao walishinda michezo mitatu mfululizo walianza vyema katika mchezo dhidi ya Everton baada ya Alexis Sanchez kupiga mkwaju safi wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari uliombabatiza mlinzi Ashley Williams na kuingia wavuni.
Everton walisawazisha na kuwa dakika chache kabla ya kwenda mapumzikoni baada ya Seamus Coleman kumalizia vyema mpira uliopigwa na mlinzi Leighton Baines.
Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa lengo la kuchukua alama tatu lakini ni Everton ndio waliofanikiwa baada ya Williams kufuta makosa yake kwa kuifungia Everton goli la pili na la ushindi.
Nahodha wa timu ya Everton Phil Jagielka alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache tu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada ya kupata kadi ya pili ya njano.
Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 34 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 37.
Everton wanabakia nafasi ya saba wakiwa na alama 23.

KAMA HUKUBAHATIKA KUANGALIA VIDEO YA SAFARI YA FRANCIS CHEKA INDIA HII HAPA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top