Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MA STAR WA KIKE WA TANO NA SIMULIZI ZA KUBAKWA...

Maisha ni safari ndefu, kila mmoja kuna wakati anapitia matukio ya kufurahisha na kusikitisha pia. Kwa mastaa imekuwa ni rahisi kubaini hasa kwa baadhi ambao wamekuwa warahisi kueleza mazuri na mabaya waliyopita katika maisha yao.
Kupitia makala haya, utaona simulizi za baadhi ya mastaa waliowahi kubakwa ama kunusurika kufanyiwa kitendo hicho!
UWOYA
Msanii wa filamu, Irene Uwoya ‘Uwoya’ anaingia kwenye orodha ya mastaa watano wenye simulizi ya kubakwa ambapo aliwahi kusimulia;
“Sikumbuki ilikuwa mwaka gani ila ni kweli nilikuwa na kama miaka 18. Nilikuwa na tabia ya kwenda na wenzangu kwenye nyumba ya mfanyabiashara mmoja aliyekuwa jirani yetu, Mbezi- Beach (naomba nisimtaje) kuangalia muvi.
“Siku moja, tukiwa kwenye sebule ya tajiri huyo ambaye ana asili ya Kihindi aliyekuwa akiishi peke yake, aliniita chumbani kwake.
“Kwa kuwa tulikuwa tumezoeana sana, sikuwa na wasiwasi wala kudhani angeweza kunifanyia jambo baya. Hee! Ile kuingia ndani si akafunga mlango, wenzangu kule sebuleni hawakujua chochote. Alichokifanya ni kunilazimisha kufanya naye mapenzi kwa nguvu, akaanza kunivua nguo, nikaona hapa nimekwisha.
“Nilichokifanya nilipiga kelele huku nikipiga ule mlango ndipo wale wenzangu walikuja na kutaka mlango ufunguliwe, jamaa alipoona kimenuka alifungua akatoka nduki na kutokomea nje.”
AUNT LULU
Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ naye ni miongoni mwa mastaa wenye simulizi ya kubakwa. Yeye anasema alibakwa na rafiki wa familia ambaye alikuwa akijitolea kumsaidia masomo yake kumbe alikuwa na lake jambo na alifanikisha lengo lake.
“Familia ilimuamini sana huyo kaka, siwezi kumtaja jina lakini baada ya kunifanyia umafya huo alikimbilia nje ya nchi mpaka leo hatujui aliko,” alisema Aunt Lulu.
KIDOA
Asha Salum ‘Kidoa’ naye anaingia kwenye skendo ya mastaa wenye simulizi ya kubakwa baada ya kukutwa na tukio moja hivi karibuni.
Ilidaiwa kuwa, akiwa kwenye studio moja iliyopo Magomeni jijini Dar alipokwenda kwa lengo la kupiga picha, alikuwa kavalia mavazi ya kimitego sana, mpigapicha uzalendo ukamshinda na kumvamia. Ila siri inabaki kwa Kidoa ambaye alipoulizwa kama alibakwa au laa alisema: “Jamani tukio hilo sipendi hata kulikumbuka maana ni jambo la aibu”
ZUWENA MOHAMED SHILOLE
Yeye amekuwa akieleza mara kwa mara jinsi alivyobakwa na mpenzi wake aitwaye Makala Elia. Shilole alisema alifanyiwa hivyo alipokuwa na umri wa miaka 16 na hatimaye akapewa ujauzito.
SANCHI
Huyu dada alianza kufahamika kwa jina la Sanchoka ila sasa anaitwa Sanchi, jina lake kamaili likiwa ni Jane Rimoy. Aliwahi kuongea na gazeti hili juzikati na kudai kuwa akiwa na umri wa miaka 6 alinusirika kubakwa, alisema:
“Ila kuna wakati huwa nalia ninapokumbuka baadhi ya matukio ambayo yaliniumiza sana. Kwanza nakumbuka nikiwa na umri wa miaka sita, nilinusurika kubakwa na rafiki wa mjomba wangu. Nisingependa kulizungumzia sana hili kwa kweli.”

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top