Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

RAIS KABILA KUONDOKA MADARAKANI MWAKA 2017...

Wapatanishi katika Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo, wameandaa mwafaka wa kuhakikisha kuwa madaraka yanapokezwa kwa njia ya amani.
Mashauriano yaliyoandaliwa na Kanisa Katoliki, yanafuatia kukataa kwa Rais Joseph Kabila, kuondoka madarakani baada ya utawala wake wa mihula miwili kukamilika.
Chini ya mapatano hayo Rais Kabila ataendelea kuwa Rais hadi wakati wa uchaguzi ifikapo mwisho wa mwaka ujao.
Waziri Mkuu mpya atachaguliwa kutoka kwa upande wa upinzani na mpango huo utasimamiwa na mkongwe wa upinzani, Etienne Tshisekedi.
Habari zinasema kuwa, ingawa kuna ripoti kuwa pande kinzani zimekubaliana kwa maswala fulani, haiwezekani sahihi za mkataba huo kutiwa sahihi kabla ya Krismasi.
Kukataa kwa Bwana Kabila kuondoka madarakani na kuahirishwa kwa uchaguzi kumesababisha maandamano makali katika barabara kuu za miji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top