Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

AROBAINI YA MTOTO WA DIAMOND, MASTAR KIBAO KUTOKA SAUZI KUHUDHURIA...



DAR ES SALAAM: Habari ya motomoto inaeleza kuwa Januari 16, mwaka huu ndiyo siku ambayo mtoto wa kiume wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ atatimiza siku 40 tangu alipozaliwa Desemba 6, mwaka jana.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa ndani ya familia ya Diamond zilieleza kuwa, Nillan ambaye ni mdogo wa mtoto wa kwanza wa staa huyo, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ anatarajiwa kufanyiwa shughuli hiyo kubwa ya kumtoa ambayo itafanyika nyumbani kwa jamaa huyo huko Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.


Taarifa nyeti zilieleza kuwa, tayari baadhi ya watu wao wa karibu Bongo wamefikishiwa kadi ambapo watakwenda Sauz na kurudi kwa usafiri maalum wa ndege ambapo kila kitu watakuwa wameshalipiwa.

“Tayari Diamond ametoa kadi maalum kwa watu wake wa karibu. Waliopewa kadi wanatakiwa kuthibitisha kama watahudhuria ili kuweka mambo sawa na kujua idadi kamili ya watakaokwenda kwa ajili ya kuwagharamia.
“Unaambiwa siku hiyo (Januari 16), watu watakula bata la kufa mtu maana shughuli ya Chibu Junior itaifunika ile ya Tiffah.
“Mbali na mastaa na watu wa kila aina kualikwa kutoka Bongo lakini pia 40 ya Chibu Junior itahudhuriwa na mastaa wakubwa Afrika ambao wengi ni rafiki zake Diamond hasa wa kutoka Nigeria,” kilifunguka chanzo chetu kikiomba chondechonde kisitajwe popote.
Staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Mbali na chanzo hicho, mtu mwingine ndani ya familia hiyo alipoulizwa juu ya taarifa za mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuhamia Sauz kwa ajili ya shughuli hiyo alisema kuwa, si kwamba tu amehamia lakini kwa sasa mzaa chema huyo ameshakuwa mwenyeji wa mitaa ya Johannesburg kufuatia kuwa huko tangu alipojifungua mkwewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Desemba 16, mwaka jana.
Hata hivyo, alipotafutwa Diamond hakuwa hewani ambapo mmoja wa wanafamilia alisema kuwa yupo nyumbani kwake Sauz kwa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2017.
“Jamaa hayupo Bongo labda umcheki kwa WhatsApp, yupo Sauz home kwake si unajua mambo ya bata za sikukuu ya mwaka mpya? Kwani kuna ishu gani?,” alihoji mwanafamilia huyo kwa sharti la kutotajwa kwani siyo msemaji wa familia ya Diamond.
Alipoulizwa juu ya 40 ya mdogo wa Tiffah na kwamba kuna mwaliko maalum na itakuwa bab’kubwa, jamaa huyo alifunguka:

“Ebana hiyo shughuli achana nayo kabisa lakini unachotakiwa kujua ni kwamba itampaisha Chibu Junior Afrika nzima.”

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top