Wakili wa zamani wa haki za kibinaadamu, Nana Akufo-Addo, ameapishwa kuwa rais mpya wa Ghana, katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi kadha wa Afrika.
Katika hotuba yake ya kwanza, Nana Akufo-Addo, alimsifu rais anayeondoka madarakani, John Dramani Mahama, kwa namna alivokiri kushindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Viongozi kadha wa Afrika walikusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kutawazwa rais mpya, Nana Akufo Addo.
Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra.
Bwana Akufo Addo, aliyewahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu, alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani.
Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.