CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewashukuru Watanzania kwa kukipa ushindi katika uchaguzi wa ubunge wa Jimbo la Dimani, Unguja, na udiwani katika kata nyingi uliofanyika Jumapili iliyopita.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, alipozungumza na wanahabari leo katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Polepole alisema kwamba mchawi wa kushindwa kwa mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) yuko ndani ya chama hicho na kisitafute kisingizio kingine.
Mgombea wa CCM huko Dimani alishinda ambapo pia chama hicho kilishinda katika kata 19 kati ya 20 ambapo moja imechukuliwa na upinzani.
“Nawashukuru sana wananchi kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi na ujio wake mpya wa Hapa Kazi Tu chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Pombe Magufuli na hivyo vyama vingine vitaendelea kukifuata chama hicho kwa nyuma,” alisisitiza katibu huyo.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.