TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo, anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na ishu ya matumizi na biashara ya madawa ya kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.