Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

E. MBASHA NA JACQUELINE MAPENZI MUBASHARA... FLORA MBASHA KULEE...



Baada ya kuficha uhusiano wao, Mwimbaji wa Gospo Bongo, Emmanuel Mbasha na Mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa, sasa siyo siri tena kwani mambo yako hazarani sasa. Mtu aliyevujisha picha zao za kimahaba, akisema kuwa, Mbasha na Jack kwa sasa hawajifichi tena kwani wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali kama kanisani, sehemu za starehe na hivi karibuni walikuwa wakijiachia Siku ya Wapendanao huku wakiwa kwenye mavazi rasmi ya wapenzi.

“Naona wameamua kuweka mambo mubashara kabisa kwa sababu Mbasha ameshasarenda kwa aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha maana sasa ni malavu kwa kwenda mbele. Ukikutana nao hata hawajifichi ,”



kilimwaga ubuyu chanzo chetu. Baada ya kupata ubuyu na picha hizo kutoka kwa sosi, mwanahabari wetu alimwendea hewani Jack ambaye muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania mkoani Kilimanjaro ambapo alifunguka kuwa, hapendi kuzungumzia kiundani mambo yake ya uhusiano lakini anachojua ni kwamba, yeye na Mbasha ni marafiki na muda ukifika, kama kuna kinachoendelea ataweka wazi kila kitu. “Muda ukifika nitaweka wazi kila kitu kama kuna mambo ya ndoa na uchumba, wala msiwe na wasiwasi ninyi mtaona tu, suala hilo huwa halina kificho,” alisema Jack kwa bashasha.

Alipotafutwa Mbasha simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu pamoja na kwamba ulionesha kupokelewa.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top