Waziri wa habari nchini Tanzania Nape Nnauye, ameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo kituo kimoja cha runinga kilivamiwa na afisa wa serikali,.
Waziri huyo wa habari amechukua hatua hiyo mara baada ya mkurugenzi wa kituo hicho cha habari, Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuambia wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho, akiwa na polisi wenye silaha.
Bw Nnauye ameunda kamati maalum ya kuchunguza kuhusu tukio hilo na akataka apewe matokeo ndani ya saa 24.
Kamera za CCTV katika kituo hicho zinamuonesha mtu anayedaiwa kuwa kamishna wa jiji la Dar es Salaam Paul Makonda (mwenye kofia), akiwa anasindikizwa na polisi waliojihami, akiingia studio za Clouds Media Group.
Rais John Magufuli amesema katika hotuba yake ya leo alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya juu eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwa Bw Makonda aendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu yeye ndiye Rais wa nchi.
Dkt Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
Taarifa zinasema kuwa Bw Makonda hakufurahishwa kuwa kituo hicho kilishindwa kupeperusha taarifa za kumchafulia jina kiongozi mmoja wa kidini.
Bw Makonda na kiongozi huyo wa dini, wametofautiana hadharani kuhusu kile kichotajwa kuwa sakata ya madawa ya kulevya.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.