Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

VITA YA SERIKALI NA MASAI SERENGETI - SERENGETI

Zaidi ya manyatta 100 za jamii ya Maasai zinadaiwa kuchomwa moto na mamlaka za mbuga ya wanyama pori karibu na mbuga ya wanyama pori ya Serenegeti.
Mamia ya watu wanaripotiwa kubaki bila makao kutokana na kuondolewa kwa jamii hii ya wafugaji. na Kijana mmoja wa kimasai anaripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.
Hii ni sehemu ya mzozo wa muda mrefu kati ya jamii ya Maasai na mamlaka ambazo huendesha shughuli za uwindaji kwa watalii.

Serikali ya Tanzania ina mipango ya kubuni eneo la ukubwa wa kilomita 1500 mraba kwenye mbuga hiyo, kwa kampuni yenye makao yake nchini Dubai ambayo hutoa huduma za uwindaji kwa watalii matajiri kutoka Milki ya nchi za kiarabu.
Mipango hiyo itasababisha watu 30,000 kupoteza makao na matatizo mengine kwa jamii ya Masai ambayo hutegemea malisho kwa mifugo wao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwani Kerry Dukunyi amesema kuwa wanavijiji wamepoteza mali katika kisa hiki cha hivi punde.
"Kiwango kikubwa cha chakula chetu kimeharibiwa... Tumepoteza chakula kingi," alisema
"Mifugo kadhaa pia haijulikani iliko."

UKO HAPA MDAADA TRUMP KWA TANZANIA...

Serikali ya Marekani kupitia ofisi ya rais Donald Trump imetangaza kupatia Tanzania ufadhili wa kukabilana na virisu vya ukimwi.
Marekani, ambayo siku chache zilizopita ilitangazatrump kusimamisha ufadhili wake kwa wizara ya afya nchini Kenya, imeipa Tanzania kitita cha dola milioni 526.
Kitita hicho kutoka mfuko wa PEPFAR, kitatumika kufanikisha mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi na virusi hivyo.
Akizungumza baada ya tangazo hilo, mwakilishi wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser amesema kuwa wanalenga kufanikisha kizazi kilicho huru kutoka virusi nchini Tanzania.
''Kwa niaba ya raia wa Marekani, tunafurahia ushirikiano wetu na Tanzania na tunajitahidi kuhakikisha hakuna anyeachwa nje," Alisema.
Miongoni mwa huduma hizo ni matibabu, ukaguzi, na kuzuia maambukizi mapya ya virusi hivyo kuanzia sasa hadi Septemba mwaka ujao.
Halikadhalika, serikali ya Marekani itashirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza huduma za kuwapima raia milioni 8.6 ili kuwawezesha kujua hali yao ya virusi.
Pesa hizo pia zitatumika kuimarisha maisha ya wajane na mayatima wa viurusi hivyo, kuzuia dhulma za kijinsia, pamoja na kuwafikia zaidi ya watu laki tatu walioambukizwa.
Mashirika mbalimbali yanayoendesha miradi mbalimbali ya afya nchini Tanzania, kama vile (TACAIDS), na wakfu wa rais mstaafu, Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF)) yanatarajiwa kushiriki kufanikisha mpango huo.
Mapema mwezi huu, Marekani ilikatiza ufadhili wake wa miradi kama hivyo nchini Kenya pamoja na kuyazuia mashirika dhidi ya kufanikisha miradi yoyote na wizara ya afya ya taifa hilo kutokana na usimamizi mbaya wa fedha.

WAHUSIKA WA 2 WA MAUAJI YA POLISI WAUAWA...

Maafisa wa polisi wa Tanzania wamewaua watu wanne wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya maafisa wanane wa polisi katika usiki wa Alhamisi kusini mwa mji wa Dar es Salaam.
Kamishna wa polisi anayehusika na uchunguzi Nsato Mssanzya amesema katika mazungumzo na vyombo vya habari kwamba wanne hao walipigwa risasi muda mfupi Ijumaa alfajiri wakati wa msako.
Maafisa waliouawa waliripotiwa kushambuliwa walipokuwa wakipiga doria katika mji huo.
Kamishna huyo alisema kuwa bunduki nne zimepatikana kutoka kwa washukiwa waliouawa ikiwemo bunduki mbili zilizoibwa kutoka kwa polisi waliouawa, huku operesheni ya kuwasaka washukiwa waliosalia ikiendelea.
Inspekta jenerali wa polisi Ernest Mangu alianzisha uchunguzi siku ya Alhamisi usiku.
Tayari rais Magufuli ameshutumu mauaji hayo na kutaka uchunguzi kufanywa.

HIZI HAPA SENTENSI 26 ZA MAGUFULI LEO APRIL 12 2017...

RAIS Dkt John Pombe Magufuli, leo Aprili 12, 2017 ameweka Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa ambayo treni ya kisasa inayotumia umeme itaweza kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya Pugu, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Rais Magufuli ameeleza haya;
  1. Nataka mkandarasi ajitahidi amalize mradi huu kabla ya miezi 30, ikiwezekana siku ya uzinduzi watu wapande bure hadi Dodoma wakashuhudie sherehe ya ofisi za serikali kuhamia Dodoma.
  2. Reli ya kisasa itarahisisha usafiri na usafirishaji wa mizigo nchini na nchi jirani za DRC, Rwanda, Burundi, Uganda.
  3. Ujenzi wa reli hiyo utakuza biashara miongoni mwa nchi zinazotuzunguka, ambapo kikwazo kikubwa kwa sasa ni miundombinu mibovu.
  4. Reli hii itakuza sekta za viwanda, Kilimo, Mifugo na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa viwandani na kwenye masoko.
  5. Treni ni njia ya bei nafuu na salama zaidi kusafirisha mizigo. hivyo tutaokoa fedha zetu ambazo hutumika kukarabati barabara.
  6. Reli itatoa ajira nyingi, wakati wa ujenzi itatoa ajira takribani laki 6, ikikamilika ajira milioni 1 kwenye za sekta mbalimbali
  7. Reli hii ya kisasa itahusisha pia ujenzi wa stesheni 6 na bandari kavu eneo la Ruvu ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
  8. Fedha za ujezi wa reli zilitengwa tangu mwezi Julai mwaka jana (2016) lakini hatukuweza kumpa mkandarasi hadi atakapoanza ujenzi huo.
  9. Rais wa Uturuki amekubali kutupa mkopo wa kujenga reli hii kutoka Morogoro hadi Dodoma na tayari ametuma wawakilishi
  10. Wale wataalam wa kusoma kwenye mitandao, wakasome nchi gani imejenga reli hii kwa fedha za ndani, ni Tanzania tu.
  11. Ukiwa dereva wa lori, hutakiwa kusikiliza watu uliowapakia wanaimba nini au wanatazama wapi, wewe endesha lori uwafikishe salama
  12. Mimi ni dereva mzuri na kwenye lori langu kuwa wanaoimba, wanaotazama nyuma, waoongea, lakini nitalifikisha ninapotaka lifike.
  13. Dereva mzuri huwa hasikilizi watu aliowapakia wanasema nini, haangalii kule wanapoangalia wao. Hili lori la maendeleo litafika.
  14. Tunajua tunapokwenda, mtu asitake kubadilisha ajenda yetu tuanze kuzungumzia mambo ambayo hayapo kwenye ilani ya chama.
  15. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi, sasa mtu amekaa kwenye ufisaidi miaka 50, huyo ni mbichi tena?
  16. Fisadi mkunje angali mbichi, akikomaa mvunje. Na wakati wa kumvunja lazima atalalamika
  17. Ninayoyafanya ni kwa niaba yenu Watanzania. Nilipozuia mchanga, sikushindwa kuwaambia na mimi wanipelekee makontena mawili Ulaya.
  18. Mimi ninawaambia Watanzania, siku moja mtaikumbuka awamu ya tano sababu ni awamu ya kazi.
  19. Tanzania ni tajiri sana, hatupaswi kuwa ombaomba lakini tumechezewa sana. Nasema inatosha tutasonga mbele
  20. Ujenzi wa reli utasaidia kutunza barabara zetu. Barabara nyingi zinaharibika sababu ya kusafirisha mizigo mikubwa.
  21. Nchi za Afrika zinachonganishwa na watu wasiojulikana halafu wanapigana wenyewe kwa wenyewe badala ya kupigania maendeleo.
  22. Nchi za Afrika zinachonganishwa na watu wasiojulikana halafu wanapigana wenyewe kwa wenyewe badala ya kupigania maendeleo.
  23. Viongozi wa vyama vya siasa, acheni CCM ifanye kazi, tukakutana 2020 lakini sasa ni kazi tu.
  24. Hapa naona mmeandika spidi itakuwa ni 160km/h, hata mkitaka fanyeni 180km/h sababu Watanzania wanapenda spidi wafike haraka.
  25. Mimi ni dereva mzuri na kwenye lori langu kuna wanaoimba, wanaotazama nyuma, wanaoongea, lakini nitalifikisha ninapotaka lifike.
  26. Niwaagize wahusika, ujenzi wa Reli ya kisasa ya Dar- Morogoro utakapoanza, ajira zote wapewe wakazi wa Pugu.

HATIMAYE RC MAKONDA ABANWA NA BUNGE... AHOJIWA DODOMA...

MKUU wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda  leo Machi 29, amebanwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo hivi punde ameanza kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hatua hiyo ya kumita RC Makonda kujibu tuhuma zinazomkabili ilifikiwa bungeni  wiki chache zilizopita baada ya kuafikiwa kwa hoja iliyotolewa bungeni na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge.

Pia Mwita alidai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.
tutaendelea kuwajuza kinachoendelea.
WENGI WANASEMA UNAFANANA NA MOYO SUKUMA DAMU... SIKILIZA MWENYEWE,,,

ALIYOYASEMA NAUYE LEO DHIDI YA RAIS MAGUFULI...

Aliyekuwa waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo nchini Tanzania Nape Nnauye amesema bado anaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kujaribu kufanikisha mageuzi nchini humo.
Bw Nnauye, akizungumza wakati wa kukabidhi rasmi afisi kwa mrithi wake Dkt Harrison Mwakyembe, kadhalika amesema ataendelea kushirikiana na wizara hiyo.
Amesema yeye ni mdau mkubwa katika sekta zilizomo chini ya wizara hiyo.
Bw Nnauye alifutwa kazi wiki iliyopita siku moja baada yake kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi kuhusu uvamizi uliotekelezwa na mtu anayedaiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika studio za kituo cha habari cha kibinafsi cha Clouds.
Kamati hiyo, kwenye ripoti yake, ilionekana kumkosoa Bw Makonda na kusema alitumia vibaya mamlaka yake.
"Heshima aliyonipa mheshimiwa Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini," alisema Bw Nnauye, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wizara ya habari na michezo Tanzania.
Taarifa hiyo inasema Bw Nnauye ameahidi ataendelea kuwa mtiifu kwa Rais Magufuli, serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Bw Nnauye, ambaye ni mbunge wa Mtama, alisimamia wizara hiyo kwa miezi 15.
Waziri mpya Dkt Mwakyembe amesema anategemea kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwa Bw Nnauye.

RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA WANAHABARI...

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa onyo kwa vyombo vya habari nchini humo kwa madai vinaandika habari zisizo za kizalendo.
Kiongozi huyo amemtaka waziri mpya wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria.
"Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue," amesema Dkt Magufuli alipokuwa anamwapisha Dkt Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Dkt Magufuli pia alimuapisha Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, na Bw Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu.
"Kwa kuwa wewe ni mwanasheria mzuri, msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia kwa sababu ya wat wachache."
"Nchi yetu huko nje ina sifa kubwa sana, juzi tu hapa amekuja rais wa Benki ya Dunia na amekubali kutupatia Shilingi Trilioni 1.74 na pia Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kutupatia fedha zingine Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, haya ndiyo mambo muhimu ya kuandika lakini hebu angalia siku iliyofuata jinsi magazeti yalivyoandika," amesema Dkt Magufuli.
Rais Magufuli ameonyesha kuchukizwa na habari zilizopamba ukurasa wa juu katika magazeti ya leo ambapo magazeti mengi yameweka picha ya aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye akitolewa bastola katika vurugu zilizotokea jana.
"Hata kasomeni tu leo magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Kwanza ukurasa wa pili, huyu anatoa anafanya hivi....nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini. Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko."
KAMA HUJASIKIA NGOMA MPYA YA MUSSA SIKAWE DAMU TULIZA MOYO, HII HAPA

NAPE AOMBA SUBIRA RIPOTI YA UVAMIZI CLOUDS MEDIA..

Waziri wa habari nchini Tanzania Nape Nnauye amewaomba wananchi nchini humo kuwa na subira kuhusu kutolewa kwa ripoti ya uchunguzi wa uvamizi uliotekelezwa katika studio za Clouds.
Bw Nnauye amesema kamati hiyo bado haijamaliza kazi yake na punde itakapofanya hivyo na kukamilisha ripoti husika, wananchi watafahamishwa.
"Kuna simu nyingi juu ya ripoti," ameandika kwenye Twitter.
"Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!"
Waziri huyo wa habari alianzisha uchunguzi baada ya mkurugenzi wa kituo hicho cha habari, Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuambia wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho, akiwa na polisi wenye silaha.

Kamera za CCTV katika kituo hicho zinamuonesha mtu anayedaiwa kuwa kamishna wa jiji la Dar es Salaam Paul Makonda akiwa anasindikizwa na polisi waliojihami, akiingia studio.
Rais John Magufuli alisema katika hotuba yake Jumatatu alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya juu eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwa Bw Makonda aendelee kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu yeye ndiye rais wa nchi.
Dkt Magufuli alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
HII HAPA NGOMA ILIYOIBUA MJADALA KUWA BABA UBAYA AMEOKOKA

NAPE AAMURU UCHUNGUZI KUVAMIWA KITUO CHA CLOUDS MEDIA

Waziri wa habari nchini Tanzania Nape Nnauye, ameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo kituo kimoja cha runinga kilivamiwa na afisa wa serikali,.
Waziri huyo wa habari amechukua hatua hiyo mara baada ya mkurugenzi wa kituo hicho cha habari, Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuambia wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho, akiwa na polisi wenye silaha.
Bw Nnauye ameunda kamati maalum ya kuchunguza kuhusu tukio hilo na akataka apewe matokeo ndani ya saa 24.
Kamera za CCTV katika kituo hicho zinamuonesha mtu anayedaiwa kuwa kamishna wa jiji la Dar es Salaam Paul Makonda (mwenye kofia), akiwa anasindikizwa na polisi waliojihami, akiingia studio za Clouds Media Group.
Rais John Magufuli amesema katika hotuba yake ya leo alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya juu eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwa Bw Makonda aendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu yeye ndiye Rais wa nchi.
Dkt Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
Taarifa zinasema kuwa Bw Makonda hakufurahishwa kuwa kituo hicho kilishindwa kupeperusha taarifa za kumchafulia jina kiongozi mmoja wa kidini.
Bw Makonda na kiongozi huyo wa dini, wametofautiana hadharani kuhusu kile kichotajwa kuwa sakata ya madawa ya kulevya.

KAMA HUJAONA VIDEO YA MU BYSER - MADHARAU... HII HAPA

JPM ATUA OFISI YA WAZIRI MKUU... KATIBU MKUU ATENGULIWA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli atengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Bw. Uledi Abbas Mussa ili kupisha uchunguzi dhidi yake.

KAMA HUJABAHATIKA KUITAZAMA VIDEO YA NURUEL - TAUSI, HII HAPA

DKT SHEIN ACHUKIZWA NA KAULI YA ZANZIBAR KUKATIWA UMEME...

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wala jana.
Matamshi yake yanajiri siku moja tu baada ya shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco kutoa ilani ya siku 14 kwa wadeni wake kwamba litawakatia moto.
Hatua hiyo ya Tanesco inajiri baada ya rais Magufuli kuiagiza Tanesco kuwakatia umeme wadeni wake wote kikiwemo kisiwa cha Zanzibar.
Makamu wa rais wa kwanza nchini Tanzania Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia.
Ziara hiyo ya Indonesia ilikuwa ya kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi ambapo alimwakilisha Rais John Magufuli.
Amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yoyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.
Dkt. Shein ameelezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema utaleta tija na faida kubwa kwa Wazanzibari na Watanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii, uvuvi, ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.
Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.

MAGUFULI AAGIZA TANESCO KUWAKATIA UMEME WASIOLIPA...

Rais wa Tanzania John Magufuli jana aliiagiza kampuni ya ugavi wa umeme nchini humo (Tanesco) kuwakatia umeme wateja wote wenye madeni makubwa kwa kampuni hiyo, ikiwemo serikali ya Zanzibar, limeripoti gazeti la The Citizen.
Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha Tanesco mkoani Mtwara, rais Magufuli alisema kuwa tasisi zote za umma zinapaswa kulipa madeni la sivyo zitakatiwa umeme.
Alisema kuwa serikali ya Zanzibar pekee , kupitia shirika la umeme za Zanzibar (Zeco), ina deni la Tanesco kiasi cha shilingi bilioni 121 za Tanzania.
"Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake.Nataka kumwambia waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu. Nikilala gizani, halafu maafisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika na sio wewe. Una hakikisho langu kwa hili.
Pesa za kulipa bili kawaida hutolewa kwa wizara zetu, lakini badala yake hupelkwa kwingine
."ninaambiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijalipa Sh121 billion. Ninyi (Tanesco) si wanasiasa...mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma...kata huduma ya umeme.Nimesema hata kama ni Ikulu , polisi, jeshi ama shule , hakuna mwenye deni anaepaswa kuachwa . Ni kwa njia hii tu tunaweza kuhakikisha kwamba pesa zilizotengewa wizara kwa ajili ya umeme zinatumiwa kama ilivyopangwa ili Tanesco iweze kuendesha kazi zake na kushughulikia matatizo ya uhaba wa umeme. ''Tanesco haiwezi kuboresha huduma kwa sababu ya madeni ya serikali yasiyolipwa''.
Alipozungumza na gazeti la Citizen jana , Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa pili wa rais , Bwana Mohammed Aboud, alisema kuwa mipango inafanyika kwa ajili ya kuliwezesha shirika la Zeco kulipa madeni ya Tanesco.
"Maagizo ya rais Magufuli yako wazi. Madeni lazima yalipwe na yatalipwa. Tumeanza mchakato wa kuhakikishwa suala hili linatatuliwa.Pia tumeiagiza Zeco kuacha kulimbikiza madeni mapya.
Mawaziri hao wawili walifanya mkutano juu ya suala hilo hivi karibuni na kujadili namna deni hilo linavyoweza kulipwa ," Bwana Aboud aliliambia gazeti la The Citizen.

RAIS MAGUFULI AAMRISHA KUTEALIWA PASPOTI MKANDARASI WA INDIA...

Rais wa Tanzania John Magufuli ameamrisha kutwaliwa kwa pasipoti ya mwanakandarasi wa India, ambaye ameshindwa kumaliza mradi wa maji kwa wakati ufaao.
Mwanakandarasi huyo Rajendra Kumar, wa kampuni ya Alliance Private Limited, alistahili kukamilisha mradi huo mwezi Machi mwaka 2015.
Lakini kulingana na waziri wa maji, alishindwa kufanya hivyo baada ya kuishiwa na pesa.
Mradi huo unaogharimu dola milioni 12.2, ni wa kuchimba visima 10 kwa manufaa ya watu 82,000 eneo la kusini mashariki mwa nchi la Lindi.
Serikali inafadhili mradi huo kwa mkopo kutoka kwa Muungano wa Ulaya na Benki ya Maendeleo ya Uerumani.
"Hatuwezi kuruhusu watu wa Lindi kuendelea kukumbwa na uhaba wa maji. Mradi huu umechelewa kwa miaka miwili kwa sababu mwanakandarasi ameamua kupeleka pesa India," alisema Rais Magufuli.
Pia aliwalaumu maafisa wa wizara ya maji kwa kuwa asilimia 90 ya pesa hizo tayari zimetumika na mradi uko mbali na kukamilishwa.

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SALMA KIKWETE KUWA MBUNGE...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Mama Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mama Salma ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa na ushawihi mkubwa sana wa kisiasa ndani ya chama chake.

MGANGA MKUU WA SINGIDA AAMUA KUACHA KAZI BAADA YA RC KUMUWEKA NDANI...


SINGIDA: Mganga  Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini, Dk. Erick Bakuza ameandika barua ya kuacha kazi ikiwa ni siku chache tangu alipopewa adhabu ya kuwekwa mahabusu na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi.
Dk. Nchimbi alitoa amri ya kukamatwa kwa daktari huyo kutokana na kuzuka ugonjwa wa kipindupindu ambao ulisababisha vifo vya watu wawili mwishoni mwa mwaka jana.
Taarifa za kuacha kazi kwa Dk. Bakuza zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Rashid Mandoa.
“Ni kweli amewasilisha barua ya kuacha kazi lakini ninavyojua mimi si kweli kwamba ameacha kazi kutokana na adhabu aliyopewa na Mkuu wa Mkoa ya kuwekwa ndani.
“Kwanza ujue hakuwekwa ndani, na ameamua kuacha kazi kwa sababu amepata sehemu nyingine ambayo anaona ina maslahi anayohitaji yeye,” alisema.
Juhudi za kumpata Dk. Bakuza kuzungumzia hatua yake hiyo hazikuzaa matunda.
Kauli ya Mkuu wa Mkoa
Wakati Mkurugenzi huyo akisema kwamba Dk. Bakuza hakuwekwa ndani, Mkuu wa Mkoa huyo, Dk. Nchimbi alithibitisha kwamba aliwekwa ndani kwa   saa tatu.
“Mimi nilitoa amri ya kukamatwa Daktari huyu na aliwekwa chini ya ulinzi kwa saa tatu. Nilimuweka ndani kwa sababu ya mazingira ambayo niliyakuta nilipokuja kuanza kuitumikia nafasi niliyoteuliwa ya ukuu wa mkoa, na nitatetea uamuzi wangu huo.
“Niliamuru akamatwe kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, kesi ya kwanza ya kuwapo kwa mgonjwa wa kipindupindu iliripotiwa Novemba 26, mwaka jana.
“Utaratibu unajulikana wazi kwamba ikifika kesi tano DMO (Mganga Mkuu wa Wilaya) anatakiwa atoe taarifa kwa MRO (Mganga Mkuu wa Mkoa).
“Desemba 4   hakutoa taarifa, ilipofika Desemba 16 vikatokea vifo viwili hakutoa taarifa hadi Desemba 18 ndipo akatangaza.
“Nikaona hakuwa makini katika kazi yake kwa sababu alipaswa kutangaza mapema ili tuchukue hatua za kudhibiti ugonjwa huo na naamini hata hivyo vifo visingetokea,” alisema.
Dk. Nchimbi alisema suala la kipindupindu halipaswi kuchukuliwa kisiasa na kwamba lenyewe lipo kitaalamu zaidi.
“Kuna taratibu ambazo hufuatwa lazima tupate evidence ya kutosha, watu wachukuliwe vipimo, yeye alinyamaza kimya. Wataalamu walipokwenda kuchunguza wakagundua kuna kipindupindu kwenye wilaya yake,” alisema.
Aliongeza: “Kwa hali hiyo niliona hakuwa makini katika kazi yake, hivyo nilitaka kumshtua tu awe makini, hakuwa makini.
“Katika hali ya kawaida angesema mapema tungechukua hatua mapema, tungetibu maji, tungesafisha visima na hata vifo visingetokea,” alisema.

KAMA HUJABAHATIKA KUIONA VIDEO YA MADHARAU HII HAPA NIMEKUWEKEA

MKUU WA WILAYA AJIUZULU KWA HIYARI YAKE...

Taarifa ambazo tumezipata kutoka Mkoani Tabora, ni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Gabriel Mnyele ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwa hiyari yake mwenyewe.
Kwa mujibu wa habari hizo, imebainika kuwa, DC Mnyele alitumia wasaha wa kuwaaga makada wa Chama cha Mapinduzi ambao walikuwa na mkutano wa kawaida hasa Madiwani wa chama hicho ambao walikuwa wakijiandaa na kikao cha Baraza.
Taarifa hizo, zimebainisha kuwa,  DC huyo alimuomba Rais John Pombe Magufuli kuwa anaachana na nafasi hiyo kwa ajili ya kwenda kufanya majukumu yake mengine.
© Copyright MO Design
Back To Top