
Watu wasiojulikana wakiwa na bastola wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao unamuunga mkono, Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na kushusha kipigo kwa baadhi ya wananchama wa CUF na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwepo mkutano huo ulipangwa kufanyika majira ya saa tano za asubuhi katika hoteli ya Vina, Mabibo lakini kabla ya kuanza waliibuka watu hao wasiojulikana wakiwa wamevalia soksi nyeusi usoni kuficha sura zao na kushusha kipigo kwa baadhi ya wanachama wa CUF waliokuwepo katika eneo hilo na waandishi wa habari.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.