
Makamu wa Rais, Samia Suluhu kesho saa mbili asubuhi ataongoza wakazi wa Arusha katika Uwanja wa Sheikh Abeid Karume kuaga miili ya wanafunzi waliofariki katika ajali ya gari Arusha ambapo serikali imegharamia sanda na majeneza kwa wanafunzi wa shule Lucky Vincent waliopoteza maisha jana kwenye ajali.

Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, amesema taarifa za awali zinaonyesha tayari serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda za kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa heikh Amri Abeid.


BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.