Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

TAMASHA LA MAHALA HAPA KUKUTANISHA WAIMBAJI KIBAO...



Muimbaji anayechipukia wa nyimbo za Injili Cliff Jasson anatarajia kuzindua album yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la MAHALA HAPA katika tamasha linalojulikana kama mahala hapa.

Akizungumza na MO Design cliff alisema kuwa siku hiyo itakuwa ndio siku rasmi ya kuiweka wakfu album yake hiyo itakayokuwa na jumla ya nyimbo 8.

Tamasha hilo litafanyika siku ya Tarehe 23-04 - 2017 katika kanisa la
DAR ES SALAAM PENTECOSTAL CHURH (DPC) lililoko Kinondoni Dar Es Salaam kuanzia saa 8:00 mchana. Hakutakuwa na kiingilio.

Waimbaji watakaomsindikiza siku hiyo ni pamoja na Bonny Mwaitege, Emmanuel Mbasha, Enock Johnas, Paster Safari, Bahati Bukuku, Beatrice Swai, Wanawake Band, Mussa Sikabwe, Catherine Madee, Hondwa Mathias, Amoni Mwakalukwa, Lusajo Sajent, Steve Njama,  Subira Mwikwabi, Shalom Group, Mc Joshua Makondeko Judia Hamis na wengine wengi.



Cliff anasema kuwa itakuwa ni siku iliyojaa utukufu kwani watu wataimba nakumsifu Mungu kwa sana. mwisho amemalizia na kuwakaribisha wote katika Tamasha hilo lililopewa jina la MAHALA HAPA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top