Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

HAYAWI SASA YAMEKUWA - PATRICIA ANAWAKARIBISHA KUSIKILIZA HII..



Mwimbaji anayechipukia katika medani ya nyimbo za Injili Patricia Ngonyani, anawakaribisha wote mnaompenda Mungu kusikiliza wimbo wake unaokwenda kwa jina la Niseme nini?
Patricia ameamua kuachia Wimbo huu kama nyia moja wapo ya kuanza kuzitangaza kazi zake za Injili ambazo zimetengenezwa katika studio maarufu nchini ya Eck Production.
Akiongea na Gospel 1 Magazine, Patricia alisema kuwa amekamilisha Albamu yake ya kwanza baada ya kupitia changamolto nyingi lakini anamshukuru Mungu kwa kuwa amemaliza salama na sasa anasubiria hatua nyingine.

"... hatua ya kwanza nimeimaliza salama japo nimepitia changamoto kadhaa, ila namshukuru Mungu kwani changamoto nilizishinda na sasa kazi ninanyo mkononi, na wimbo huu wa niseme nini nimewawekea hapo ili msikilize kile nilichokuwa na kifanya..." alisema Patricia

aliendelea kusema kuwa, sasa yupo katika maandalizi ya hatua nyingine ambayo ni kufanya Video za albumu yake hiyo. ambayo inajumla ya nyimbo nane ambazo ni, Uwepo Wako, Uhimidiwe, Peleleza, Nchi, Niseme Nini, Mpeni Bwana, Nalitafakari Jina na  Umeona.

AUDIO HII HAPA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top