Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MAWAKILI UINGEREZA WATAKA MAGUFULI KUCHUNGUZA SHAMBULIO LA LISSU...

Chama cha mawakili na watetezi wa haki za kibinaadamu nchini Uingereza wamemuandikia rais John Pombe Magufuli wakimtaka kuanzisha uchunguzi ulio huru mara moja kuhusu jaribio la mauaji lililotekelezwa dhidi ya mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu.
Wakili huyo ambaye pia ni rais wa chama cha mawakili nchini Tanzania TLS mnamo tarehe 7 mwezi Septemba alipigwa risasi tumboni na miguuni na watu wasiojulikana katika makaazi yake ya Dodoma.
''Ufyatulianaji huo wa risasi na maswala mengine ambayo yemetokeo yanayowahusisha mawakili yanatia wasiwasi''.
Ni muhimu sana kwamba chama cha mawakili kinaheshimiwa kwa kuwa ni kitengo muhimu katika kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa kikamilifu, ilisema barua hiyo.
Barua hiyo ilisainiwa mnamo siku ya Jumatano na rais wa chama cha mawakili Joe Egan ,mwenyekiti wa baraza hilo Andrew Langdon na Mmwenyekiti wake Kirsty Brimelow.
Mawakili hao wamemwambia rais Magufuli pia kuanzisha uchunguzi kuhusu visa vingine vya uhalifu vinavyotekelezwa dhidi ya mawakili.
Visa hivyo ni pamoja na mlipuko katika afisi ya mawakili ya IMMMA chini ya mwezi mmoja na tisho la waziri wa maswala ya kikatiba na sheria Harrison Mwakyembe la kutaka kufutilia mbali chama cha mawakili nchini Tanzania katika kipindi cha miezi saba iliopita.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top