Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ILIVYOTOKEA TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI...



habari kutoka kwa moja wa vyanzo vyetu zinasema kuwa Mh. Tundu Lissu alianza kufuatiliwa  alipotoka Bungeni.
chanzao hicho ambacho ni Mbunge wa Rombo Joseph Selesini, amesema kuwa taarifa alizozipata ni kuwa Mh. Lissu alikuwa alikuwa akifuatiliwa na gari toka alipotoka Bungeni na Dereva wake alilishitukia hilo.
alisema kuwa Dereva alipoona wanafuatiliwa alilipeleka gari mpaka nyumbani, na walivyofika nyumbani alimsihi Mh. Lissu asishuke kwanza kwenye Gari.
" watu hao walipoona hawashuki, walijifanya kuna kitu wanaangalia, na walipoona kuna hali ya utulivu, walisogeza gari lao ambalo lilikuwa na vioo vyenye giza na kuanza kumimina risasi upanda aliokalia Mh. Lissu." 
amesema.
habari zinasema kuwa Mh. Lissu alipigwa risasi Mguuni, Mkoni na Tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri.
Tundu Lissu amepigwa risasi leo na alhamisi na watu wasiojulikana na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya Dodoma
lakini tayari taratibu zilishafanywa kwaajili ya kumuhamishia Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top