Mwanasiasa wa upinzani na Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu ameripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Tanzania.
Mwanasiasa huyo amekimbizwa hospitali ya Dodoma General baada ya kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake Jjijini Dodoma Tanzania
Chama Cha Chadema kimeshutumu vikali tukio hilo.
Hivi karibuni, Tundu Lissu amekuwa akikamatwa mara kwa mara na polisi akishutumiwa kufanya uchochezi.
Akithibitisha tukio hilo,kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Mh. Zitto Kabwe (Mb) amesema " Tundu Lissu yupo hospitali, na bado anajaribu kupambana kuokoa maisha yake"
Gazeti la Mwananchi nchini, limemnukuu Mganga mkuu wa hospitali ya Dodoma amesema kuwa Tundu Lissu ana majeraha ya risasi miguuni na tumboni.
Endelea kuperuzi MO Designtz kwa Habari zaidi juu ya Tukio hili.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.