NYUMBA ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) iliyopo Mwandiga, mkoani Kigoma yateketea kwa moto.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa, nyumba hiyo aliijenga wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza na ipo Kibingo, Kata ya Mwandiga, Mjini Kigoma.
Msaidizi wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba Zitto hakuwa anaishi kwenye nyumba hiyo.
Amesema Zitto alihama kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyumba nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho hicho na iliyoungua na ilikuwa ikitumika kwa dharura.
Kwa upande wake, Mohammed Babu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya ACT Amani (Ulinzi na Usalama) amesema wao kama chama wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko, na bado wanaendelea na kufuatilia, taarifa zikikamilika watawajulisha wananchi.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.